Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Felix Maagi
akiiongoza Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakati ilipotembelea
eneo la mradi wa nyumba ambao unatarajiwa kuanza katika uwanja wa
kulenga shabaha wa jeshi la wananchi Kunduchi, baada ya makubaliano kati
ya jeshi la wananchi na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kamati hiyo
ikiongozwa na mwenyekiti wake na jimbo la Kahama Mbunge Mh. James
Lembeli na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa
Anna Tibaijuka ilitembelea eneo hilo ili kujiridhisha na kujionea hali
halisi na kupata maelezo ya kina kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mradi
huo. Kulia ni Mjube wa Kamati hiyo Mh. Hamud Jumaa na Mbunge wa jimbo la
Kibaha Vijijini, kulia ni James Lembeli Mbunge wa Kahama na Mwenyekiti
wa kamati hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Isaack
Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa NHC akielekeza
jambo wakati alipokuwa akionyesha eneo hilo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na wajumbe wa kamati
hiyo wakati alipotembelea eneo hilo huku Kunduchi. Mjumbe
wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili Mh. Hery
Shekifu akifafania jambo huku Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli
wakimsikililiza Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh.
James Lembeli akizungumza jambo wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo la
kulenga shabaha la jeshi Kunduchi, kulia ni Mama Zakhia Megji
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC na kushoto ni
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna
Tibaijuka Baadhi
ya watendaji na maofisa wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC wakiwa katika
picha ya pamoja kwenye uwanja wa Kulenga Shabaha wa jeshi Kunduchi
ambao kwa sasa matumizi yake yanabadilisha na kuwa mradi wa nyumba za
Shirika la Nyumba la NHC. Baadhi
ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na
Mazingira wakishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la
Tanganyika Pakers ambapo mradi wa Kawe City unatarajiwa kuazishwa na
shirika hilo la NHC. Huu ndiyo uwanja wa Kulenga Shabaha wa jeshi Kunduchi mahali ambapo sasa panaanzishwa mradi wa nyumba za NHC. Waziri
wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka
akishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la Tanganyika
Pakers Kawe jijini Dar es salaam leo. Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na
mbunge wa Kahama Mh. James Lembeli akishuka kwenye gari katika eneo la
Tanganyika Pakers mahali ambapo patatekelezwa mradi wa Kawe City
unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC. Waziri
wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka
akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli katikati ni mjumbe wa kamati
hiyo na Mbunge wa jimbo la Lushoto Mh. Hery Shekifu Isaack
Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa NHC akendelea
kutoa maelezo kwa kamati hiyo wakati ilipotembelea katika eneo la
Tanganyika Pakers Kawe. Wajumbe
wa kamati hiyo wakipata maelezo kabla ya kuanza ziara yao leo katika
makao makuu ya shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga jijini Dar es
salaam. Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh.
James Lembeli akizungumza wakati kamati hiyo ilipokuwa ikipata maelezo
ya awali kabla ya kutembelea maeneo yatakapotekelezwa miradi hiyo
mikubwa ya makazi , Kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya
Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na kutoka kulia ni Mh. Mary Mwanjelwa
mjumbe wa kamati hiyo na mbunge wa viti maalum Mbeya mjini na Mh. Abdulkarim Shah Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo na na Mbunge wa Mafia. Kutoka
kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la NHC
Mh. Zakhia Megji, Bw. Felix Maagi Kaimu Mkurugenzi wa NHC na Mbunge wa
jimbo la Ubungo na mjumbe wa kamati hiyo Mh. John Mnyika ambaye
naonekana akitoa mchango wake wakati wa wajumbe hao walipokuwa wakipata
taarifa ya awali..
No comments:
Post a Comment