Meneja wa
Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa akizungumza na waandishi wa
habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mbio za Mitumbwi Kanda
ya Ziwa, zijulikanazo kama “Balimi Boat Race”
iliyofanyiak Dar es Salaam jana.
*****************************************
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra leo imetangaza
rasmi kudhamini kwa mara nyingine tena mashindano ya mbio za mitumbwi kwa
wakazi wa kanda ya ziwa kwa mwaka huu wa
2014. Mashindano haya ya “kupiga
makasia” yanafanyika kwa mwaka wa kumi na tano sasa na yamekuwa na hamasa
na msisimko mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam
leo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra
Lager, Edith Bebwa alisema kwamba lengo hasa la Bia ya Balimi Extra
kudhamini mashindano haya ni kufurahi pamoja na wakazi wa kanda ya ziwa
hususani wale ambao ni wavuvi. Aliendelea kusema, “Mashindano haya yanaenzi na
kulinda tamaduni zetu zisipotee, yanajumuisha watu mbalimbali kukutana,
kufahamiana na kufurahi kwa pamoja na hii inasaidia sana kuimarisha amani na upendo
baina yetu. Amani ni nguzo muhimu sana kwa Taifa letu”. Alisisitiza pia umuhimu
wa michezo katika kujenga afya bora.
Edith alifafanua kwamba kwa mwaka huu mashindano ya mitumbwi
yatahusisha miji mitano ya kanda ya ziwa kama ratiba inavyoonyesha hapo chini
kwa hatua ya awali.
TAREHE
|
MAHALI/MKOA
|
UWANJA
|
18/10/2014
|
KIGOMA
|
UFUKWE WA MAGEREZA
|
01/11/2014
|
BUKOBA
|
UFUKWE WA SPICE BEACH
|
08/11/2014
|
MWANZA
|
UFUKWE WA MWALONI
|
15/11/2014
|
KISIWA CHA UKEREWE
|
UFUKWE WA HOTELI YA MONARCH
|
22/11/2014
|
MUSOMA
|
UFUKWE WA BWALO LA POLISI
|
Washindi watakaopatikana katika miji hii watashindanishwa
kwa pamoja ili kumpata mshindi wa kanda. Shindano la kumpata mshindi wa kanda
linategemewa kufanyika jijini Mwanza mwanzoni mwa mwezi December. Tarehe 6
Disemba 2014.
Edith Bebwa akizungumzia zawadi za mwaka huu alisema kwamba
katika ngazi ya mikoa na ngazi ya kanda Balimi Extra imetenga zaidi ya shilingi
milioni ishirini na nne kama zawadi za pesa taslimu kwa washindi. Mpangilio wa
zawadi ni kama inavyoonekana hapa chini;
ZAWADI
|
NGAZI YA MKOA
WANAUME
|
NGAZI YA MKOA
WANAWAKE
|
NGAZI YA KANDA
WANAUME
|
NGAZI YA KANDA
WANAWAKE
|
Mshindi wa Kwanza
|
900,000
|
700,000
|
2,700,000
|
2,300,000
|
Mshindi wa Pili
|
700,000
|
600,000
|
2,300,000
|
1,700,000
|
Mshindi wa Tatu
|
500,000
|
400,000
|
1,700,000
|
900,000
|
Mshindi wa Nne
|
400,000
|
300,000
|
900,000
|
700,000
|
Mshindi wa 5 - 10
|
6 @
250,000
|
6 @
200,000
|
6 @
400,000
|
6 @ 250,000
|
Edith alimaliza kwa kuwaomba wanachi wa kanda ya ziwa
wajitokeze kwa wingi katika miji iliyotajwa ili kufurahi kwa pamoja katika
matamasha haya. Alisisitiza wasisahau mila na tamaduni zao katika kipindi
ambacho watu wengi hupenda kuiga tamaduni za kimagharibi. Alimaliza kwa
kuwashukuru sana wanywaji wa bia ya Balimi Extra kwa kuchagua bia hii na kuomba
waendelee kuitumia kwani ni kupitia mchango wao ndipo pia Balimi Extra Lager
inaweza kuleta burudani kama hizi kwa ajili yao.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na;
Arthur Kanza, Balimi Extra
Lager Brand Manager, simu; +255 767 266 717,
Kuhusu TBL;
Tanzania
Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye
ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania.
TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni
shiriki ya Mountainside Farms Limited.
Bia
zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro
Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine
vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream,
Redd’s Premium Cold na Grand Malt.
Kundi
la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam,
limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya
bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari
nane za kusambazia bia.
Kuhusu SABMiller;
SABMiller
plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya
kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia
zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro
Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko
ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya
makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni
SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za
uzalishaji nchini India. SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya
London na Johannesburg.
No comments:
Post a Comment