Mmoja ya wasicha walioathirika na madawa ya kulevya na sasa yupo katika kituo |
Serikali na
Taasisi zisizo za kiserikali zimetakiwa kusaidia nyumba za malezi za waathirika wa dawa za kulevya
ili ziweze kuwahudumia watumiaji wa dawa
hizo wasiokuwa na uwezo.
Ombi hilo
lilitolewa jana na Frank John ambaye ni Meneja wa nyumba ya South Beach iliyopo
Kigamboni kwenye hafla ya waathirika wa dawa
hizo za kulevya wanaoelelewa kwenye kituo hicho kukaa mwaka mmoja bila
ya kutumia dawa za kulevya za aina yoyote ile.
“Lengo la nyumba
hizi za malezi ni kupambana kuwatoa vijana hawa waliothirika na dawa za
kulevya katika hali ya uteja na kurejea
katika maisha ya kawaida ili waweze kujitambua, kujiendeleza na hatimaye
kutimiza ndoto zao walizokuwa nazo awali kabla hawajatumia dawa hizo.”Alisema
John.
John alisema yeye alitumia dawa hizo za kulevya kwa
miaka 18 kutokana na vishawishi vya marafiki na kwamba siyo rahisi na wala
haikuwa rahisi kwao kufikisha mwaka
mmoja na zaidi bila ya kutumia dawa za
kulevya za aina yoyote bila ya kuwa na
watu wa kuwasaidia na kuwaunga mkono.
Rashidi Nassoro ambaye
alitumia dawa hizo za kulevya kwa muda
wa miaka sita na sasa amefanikiwa kuishi bila ya kuyatumia, alisema mtumiaji wa dawa za kulevya ’teja’ ili aweze kupata matibabu ni gharama na
kwamba matibabu yao yanachukua kipindi cha miezi minn ne na kwamba wengi wao
wanashindwa.
Hivyo aliomba serikali,
taasisi zisizo za kieserikali na wazazi wasiwanyanyapae, wawasaidie ili kuweza
kuepuka maisha ya utumiaji wa dawa za kulevya kwa sababu ni maisha magumu,
yenye vishindo na yasiyoisha mateso.
Aliongeza kuwa
matibabu hayo yanawasaidia kupata nafuu ila iwaomba watumiaji waendelee
kuhudhuria kwenye nyumba hizo za malezi na kuachana na marafiki wenye
vishawishi ili wasije wakarejea tena kwenye matumizi hayo.
Kwa upande wa
msichana Nesha Mfinanga alisema wamewaumiza wengi ikiwamo familia
kutokana na matumizi wa dawa hizo za kulevya
na kwamba tangu apate matibabu
hayo anajitambua na kujutia makosa na muda alioupoteza wa kipindi cha miezi 9
na kuiomba jamii isiwanyanyapae iwasaidie watabadilika na kutimiza ndoto zao.
No comments:
Post a Comment