Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kiongozi wa
Bendi ya Msondo Ngoma,Mzee Said Mabela.
*******************************
Bendi
Kongwe ya Muziki wa Dansi hapa nchini iliyodumu kwa miaka 50 toka
kuanzishwa kwake mwaka 1964,Msondo Ngoma Music Band imesherehekea
jubilei yake hiyo iliyofanyika Novemba 1,2014 katika viwanja vya TCC
Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha mashabiki wake
lukuki kutoka sehemu mbali mbali.
Mgeni
Rasmi katika Sherehe hizo za kusherehekea Jubilei ya miaka 50 ya Bendi
ya Msondo Ngoma,alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye
aliweza kuwatunuku vyeti vya heshima wanamuziki mbali mbali walioitumia
Bendi hiyo toka ilipoanzishwa mpaka sasa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof.
Elisante Ole Gabriel akipokea Cheti cha heshima kutoka kwa Muwakilishi
wa Mfuko wa PSPF,Abdul Njaidi ambao ni sehemu ya Wadhamini wa Bendi hiyo
ikiwa ni sehemu ya heshima kwa Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa
mchango wake mkubwa kwa wasanii mbali mbali hapa nchini.Cheti hicho
kimetolewa na Bendi ya Msondo Ngoma.Picha Zote na Othman Michuzi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima mpiga solo
hodari wa Bendi ya Msondo Ngoma,Abdul Ridhwan "Panga mawe"
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof.
Elisante Ole Gabriel akimkabidhi Cheti pamoja na fedha taslim sh. Laki
5,Mke wa Marehemu Mzee Muhidin Maalim Gurumo katika hafla hiyo ya
kutimiza miaka 50 ya kuanziswa kwa Bendi hiyo.
Mmoja
wa Waanzilishi wa Bendi hiyo,John Simon (Kapten Mstaafu) akizungumza
machache pamoja na kutoa historia fupi ya kuanza kwa bendi hiyo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti pamoja fedha taslim sh.
Mil. 5,Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) kwa
niaba ya baba yake.
Mtangazaji
Mkongwe hapa nchini na mwenye historia na Muziki wa Tanzania,Masoud
Masoud (kulia) akionyesha moja ya CD za bendi ya Msondo Ngoma zilizokuwa
zikinadiwa kwenye sherehe hizo mbele ya Wadhamini.
Safu
ya waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma ikiongozwa na Nguli Shaaban Dede
(katikati) wakifanya vitu vya mbele ya mashabiki wao lukuki waliofika
kwenye Viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.
Mpiga Tumba wa Msondo Ngoma akifanya yake.
Hassan
Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) akionyesha uhodari
wake kiasi kwamba hata pengo la mzee wake kuhisi limezibwa.
Rapa wa Bendi ya Msondo Ngoma,Roman Mng'ande akifanya mambo.
Baba la Mababa,Mzee Said Mabela akiendeendelea kuzikonga nyoyo za Mashabiki wa Msondo. Picha kwa hisani ya Othman Michuzi
No comments:
Post a Comment