Waziri wa Ujenzi Dr.John Pombe Magufuli Kituo cha BRT kivukoni jijini Dar es salaam leo akiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Mkurugenzi Mkuu wa DART Asteria Mlambo (kulia) akimwongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiki anayefuatana na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kuegesha mabasi ya haraka kinachojengwa eneo la Jangwani, jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari (aliyeshika kijiti) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi kuhusu utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam
Kampuni
ya Strabag International GmbH inayotekeleza ujenzi wa barabara ya
Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni hapa jijini Dar es Salaam
imetakiwa kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya
kipindi cha miezi sita ijayo kama mkataba wao unavyoelekeza.
Waziri
wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara ya
kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi
yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit -
BRT) ambao umeelezewa kuwa na changamoto nyingi kiasi cha kusababisha
usumbufu kwa watumia barabara hiyo kwa kipindi kirefu.
Akimpatia
taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi
Patrick Mfugale alimjulisha Waziri Magufuli kuwa kwa hivi sasa
changamoto nyingi zimefanyiwakazi na mradi unaendelea kusimamiwa kwa
karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna ucheleweshaji zaidi katika hatua hii
iliyobaki. Mkataba
wa ujenzi wa barabara hizi pamoja na vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi
Desemba mwaka 2012 ukiwa umepangwa kukamilika katika kipindi cha miaka
mitatu kwa gharama ya Shilingi bilioni 280.
Kwa
upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Saddik
ambaye aliambatana na Waziri Magufuli katika ziara hiyo, amewataka
wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao ndani ya sehemu ambayo
mkandarasi anaendelea na kazi waondoke kwani hiyo mbali ya kuwa kinyime
na taratibu za uendeshaji biashara zilizowekwa lakini pia imekuwa ni
moja ya kisingizio kinachotolewa kwamba uendeshaji wa shughuli hizo
unachangia kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo.
Waziri
Magufuli akizungumza wakati wa kuhutimisha ziara hiyo, amemtaka
mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha mradi huo kwa muda na viwango
vilivyokusudiwa.
“Na
kwa wale walio ndani ya eneo la ujenzi ni lazima sheria ichukue mkondo
wake” alisisitiza Waziri Magufuli huku akimtaka Mkurugenzi wa Manispaa
ya Kindondoni Mhandisi Mussa Natty kuhakikisha anasimamia zoezi hilo la
kuondoa haraka wale wote wote walioingia katika eneo hilo la barabara
kinyume na sheria.
Aidha,
Waziri Magufuli alielezea kushangazwa kwake kwa kuchelewa kuondolewa
kwa nyaya za Tanesco katika maeneo ya City Squire na Morocco kwani fedha
za kutekeleza kazi hiyo tayari zimelipwa muda kirefu.
“Ucheleweshaji
wa ainaa hii ndiyo unaotoa mwanya kwa mkandarasi kuanza kutoa
visingizio vya kutokamilika kazi hii kwa wakati” ametahadharisha Mhe.
Magufuli.
Hata
hivyo katika hatua nyingine Mhe. Magufuli amemtaka mkandarasi
kuharakisha taratibu za kuifungua barabara hiyo upande wa kuingia Dar es
Salaam ambako kwa sasa hivi hakuna shughuli kubwa zinazofanyika ili
kupungiuza adha ya msongamano wa magari yanayopishana katika njia moja
ya upande wa kutokea mjini katika barabara hiyo ya Morogoro hasa kwa
eneo kati ya Ubungo na Kiamara.
Naye
Msimamizi wa mradi huo kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari
ameelezea kuwa, utekelezaji wa mradi huu wa usafiri wa haraka utajengwa
katika awamu sita. Awamu
ya kwanza ambayo ujenzi wake ndio huu unaoendelea inahusisha barabara
zenye jumla ya kilometa 20.9 ambazo ni Kimara – Kivukoni, Magomeni –
Morocco na Faya – Karikaoo. Hadi sasa mkandarasi amekwisha kamilisha
asilimia 55 ya mradi
No comments:
Post a Comment