Picha
juu na chini ni Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa,
Pierre-Yves Ginet akizungumza na wanafunzi wa shule za sekondari
mbalimbali za jijini Dar es Salaam na kuwaonyesha picha na kuwapa
ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayo wakinamama wamekuwa wakifanya kwa
mustakabali kwa kuleta usawa na haki za wanawake duniani.
Shirika
la Ufaransa la Alliance Francaise de Dar es Salaam liliandaa safari ya
maonyesho iliyopewa jina “women in Resistance by the talented French
photo-journalist Pierre-Yves Ginet.
Mwandishi
wa habari huyo mpiga picha Pierre-Yves Ginet ambaye alifanya kazi ya
kutafuta wanawake wanaojituma katika maisha yao ya kila siku na kazi
zake zimeweza kuwapa ari na moyo wakinamama wengi Afrika.
Kati
ya 2001 na 2006, alisafiri zaidi ya nchi 17 akipiga picha za wakinamama
ambayo katika shughuli zao waliweza kufungua ukurasa mpya na
kubadilisha historia katika kizazi cha leo.
Katika
shughuli na katika njia tofauti walizotumia katika kubadilisha maisha
wa wakinamama wengi duniani, wanawake kupitia kazi za picha Ginet
wameweza kuwa na dhamira moja kubwa nayo ni kubadilisha maisha ili
kuweza kuwa matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi kwa sasa na baadaye.
Maonyesho
hayo ya lengo la kuwapa usawa wakinamama wote kupitia mabara yote hapa
duniani na hasa nchi zinazoendelea, sehemu za vita.
Na
sehemu kubwa ya picha hizo zinaonyesha jinsi wakinamama wanavyopambana
ili kujikwamua katika unyonge na ukandamizaji wa aina yoyote hapa
duniani. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
No comments:
Post a Comment