Bondia Kalama Nyilawila katikati akitia saini ya kucheza pambano siku ya mei mosi atacheza na Thomasi Mashali au Japhert Kaseba inategemea na mshindi wa mechi hiyo ya March 29 itakayofanyika PTA Sabasaba kulia ni Alli Mwazoa na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Promota wa ngumi nchini Ali Mwazoa akipeana mkono na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi baada ya kumsainisha bondia Kalama Nyilawila katikati anaetarajia kuzipiga mei mosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Promota wa ngumi nchini Ali Mwazoa akipeana mkono na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi baada ya kumsainisha bondia Kalama Nyilawila katikati anaetarajia kuzipiga mei mosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Na Mwandishi Wetu
Bondia Kalama Nyilawila Ameingia mkataba
wa makubaliano na promota Ali Mwazoa wa Tanga kwa ajili ya mpambano wa
Mei Mosi mwaka huu ambapo anasubili mshindi wa mpambano kati ya Thomasi
Mashali na Japhert Kaseba ambao watazichapa March 29 katika ukumbi wa
PTA Sabasaba ambapo mshindi atacheza na
Kalama Nyilawila siku ya mei mosi akizungumza baada ya kusaini mkataba
huo bondia Kalama Nyilawila alijitapa kwa kusema iwe Mashali awe Kaseba
yoyote atakae kutana nae ato kuwa na masiara nae atampiga kipigo cha
mbwa mwizi kwani nafasi hiyo alikuwa anaitafuta siku nyingi baada ya
kupoteza huwezo wake katika masumbwi hivyo sasa wakae mbali na mimi
kwani nakuja kwa nguvu mpya kabisa akisema atakuwa hatari kama 'Mbeya
City' timu ambayo inatoka mkoani kwao na kufanya maajabu kwa kuitawala
ligi kuu ya Tanzania bara ndivyo na mimi nitakavyofanya
Kalama katika harakati zake za
kuhakikisha anarudi katika chati kama zamani mechi yake ya mwisho katika
kuukaribisha mwaka 2014 alimsambalatisha bondia Ibrahimu Maokola bila
huruma kwa kumpiga K,o ya raundi ya pili mpambano uliofanyika katika
ukumbi wa Msasani klabu
Nae promota wa mpambano huo Mwazoa
amesema kila kitu kinaendelea vizuri ikiwemo mapambano ya utangulizi
yenye mabondia bora wanaotamba kwa sasa ambao wapo kwenye kiwango cha
ali ya juu kwa kuwa mwaka huu ni wa masumbwi nchini Tanzania nimeanza na
nitaendelea kusapoti na kupromot mchezo wa ngumi popote nchini
akizungumza kwa niaba ya chama
kilichopewa dhamana ya kusimamia mchezo huo wa mei mosi Rais wa TPBO
Yassini Abdallah 'Ostadhi' amesema watanzania wana bahati sana kwa
kujitokeza promota mwenye uchu wa maendeleo kwa mabondia kwana mabondia
wote wame saini mkataba na kupewa posho ya kufanyia mazoezi isipokuwa
bondia mmoja tu kati ya watakaocheza march 29 ni Kaseba au Mashali jibu
ndio tunasubili siku hiyo nani zaidi na atakaepata nafasi ya kuchapana
na Kalama
No comments:
Post a Comment