Mabondia
Thomas Mashali (kushoto) na Japhet Kaseba wakitambulishwa na Promota wa
pambano lao baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kucheza pambano
lao la ubingwa wa Mabaara wa 'Universal Boxing Organization' (UBO)
pambano litakalopigwa tarehe 29 machi 2014 katika ukumbi wa Karume,
zamani ukiitwa PTA hall.
Pambano
hilo limeandaliwa na mratibu Ally Mwanzoa na zoezi la kupima afya
lilifanyika jana katika ukumbi wa Vijana Kinondoni, jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari kiongozi
wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim kamwe aliyefatana na Anthony ruta
amesema makubaliano yamekwenda vizuri na wote wametia saini kucheza
pambano hilo litakalopigwa katika uzani wa kilogram 79 na wamechukua
malipo yao ya awali kuashiria kuwa pambano hilo lipo na kila mmoja
amejigamba kumchakaza mwenzake siku hiyo na kujitengenezea mazingira
mazuri katika ubingwa wake huo.
Baadhi ya waliohudhuria zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment