Vyama
vya Mpira wa Miguu vya mikoa vimetakiwa kuwasilisha majina ya mabingwa
wao kufikia Machi 30 mwaka huu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa
(RCL).
Timu
zote zitakazofuzu kucheza RCL zinaruhusiwa kusajili wachezaji wapya
wasiozidi watano kutoka ndani ya mkoa kwa kufanya taratibu za uhamisho.
Kamati imesisitiza kuwa usajili wa RCL ni uleule uliotumika kwenye Ligi
ya Mkoa.
Kamati
ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
iliyokutana Februari 6 mwaka huu imekataa ombi la Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) kuongeza timu za Ligi ya Mkoa kutoka 20 hadi
24.
Ikiwa
chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange, Kamati hiyo imesema kwa mujibu
wa Kanuni ya Ligi ya Mkoa, ligi hiyo inatakiwa kuwa na timu kati ya 16
na 20, hivyo vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vinatakiwa kuendesha
ligi kwa kufuata kanuni.
Kamati
hiyo imeongeza kuwa hata kama ingekubalia ombi la MZFA kiutaratibu
lisingewezekana kwa vile kanuni hufanyiwa marekebisho baada ya msimu
kumalizika, wakati ombi hilo limewasilishwa katikati ya msimu.
No comments:
Post a Comment