Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe, akiwasili
kwenye ofisi za Makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini, leo asubuhi kwa
ajili ya kuhojiwa kuhusu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa chama
hicho hivi katibuni, ya kuwa watafanya maandamano nchini nzima bila
kikomo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),John Mnyika
akizungumza na waandishi wa habari wakati walipowasili eneo la makao
makuu ya Jeshi la Polisi.
Makamu
Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa Chama,Wakili
Mabele Marando wakiwasili Makao Makuu wa Jeshi la Polisi mapema leo.
Baadhi
ya Wachama na Wafuasi wa Chadema wakishangilia wakati Mwenyekiti wao
akiwasili kwenye Makao Makuu ya Jeshi la Palisi leo.
Kamishna
wa Polisi,CP Paul Chagonja akitoa akiwataka wanachana na wafuasi wa
Chadema kuondoka kwenye eneo hilo kwani hakuna sababu ya kufanya fujo.
Ulinzi mlali katika eneo hilo. Picha na Othman Michuzi.
No comments:
Post a Comment