Mke wa
Waziri Mkuu,MamaTunu Pinda akipokea kiasi cha dola elfu moja kutoka kwa
Mkurugenzi wa Masoko utafiti na huduma kwa wateja wa Benki ya
CRDB,Tully Esther Mwampamba kama mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa
Kanisa la kiinjili Moroviani Tanzania (KKMT) Mburahati jijini Dar es
salaam.kulia ni Askofu David Martin Mwalyambile wa kanisa hilo Mama
Pinda alikuwa mgeni rasimi katika kuendesha harambee ya kuchangia
ujenzi wa Kanisa hilo ambapo kuliweza kupatikana kiasi cha shilingi
milioni mia moja na ishirini na nane.Picha na Chris Mfinanga
Mke wa
Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akimshukuru mtoto Cecylia Mashaka Mwaisaka
mwenye umri wa miaka mitatu kwakuchangia shilingi elfu ishirini kama
mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Moroviani mburahati
jijini Dar es salaam.Mama Pinda alikuwa mgeni rasimi katika kuendesha
harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo ambapo kuliweza kupatikana
kiasi cha shilingi milioni mia moja na ishirini na nane.
Kwaya ya kanisa la Moroviani Mburahati ikitumbuiza katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa Kanisa lao.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment