Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiingia kwenye kwenye ukumbi wa Hoteli ya
Serena kwa ajili ya chakula cha jioni cha kampeni za kupambana na
utumikishwaji wa mtoto hapa nchini kilichoandaliwa na Shirika la
International Rescue Committee tarehe 5.9.2014.
Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akisalimiana na Msanii maarufu wa kimataifa Daniele de
Niese anayetumiwa na Shirika la International Rescue Committee katika
kuhamasisha mapambano ya utumikishwaji wa watoto.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania
kwenye Umoja wa Mataifa Dkt Augustine Mahiga wakati wa chakula cha
jioni kilichoandaliwa na International Rescue Committee kwenye hoteli ya
Serena tarehe 5.9.2014 kwa ajili ya kuhamasisha mapambano dhidi ya
utumikishwaji wa watoto hapa nchini.
Msanii
wa Kimataifa anayetumia kipaji chake cha kuimba Daniele de Niese
akiimba nyimbo mbalimbali kwa lugha mbalimbali, kiingereza, kifaransa,
kitaliano wakati wa chakula cha jioni katika kuhamasisha mapambano dhidi
ya utumikishwaji wa watoto.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza msanii wa kimataifa Daniele de
Niese mara baada ya kutumbuiza kwa nyimbo zake za kusisimua kuhusu
mapambano dhidi ya utumikishwaji wa watoto wakati wa chakula cha jioni
kwenye Hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014.
Mtoto
Hamadi Hatibu, 13, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi ya
Sahare katika Manispaa ya Tanga akitoa ushuhuda wake jinsi alivyoishi
kwa kuvua samaki katika umri wake mdogo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa chakula cha jioni cha
kampeni za kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa Tanzania
kilichoandaliwa na International Rescue Committee kwenye Hoteli ya
Serena tarehe 5.9.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi kampeni ya kadi nyekundu
katika kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa Tanzania wakati wa
chakula cha jioni kilichoandaliwa na International Rescue Committee
katika Hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Msanii wa Kimataifa
Daniele de Niese mara baada ya kuzindua rasmi kampeni za kupambana na
utumikishwaji wa mtoto hapa Tanzania.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na mtoto Hamadi Hatibu aliyekuwa mwathirika wa utumikishwaji wa mtoto.
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment