TAMASHA la ‘Coastal Day’ limefanyika leo katika
uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga ambapo mashabiki na wanachama wa klabu hiyo
wamepata nafasi ya kuwaona wachezaji wapya waliosajiliwa majira ya kiangazi
mwaka huu.
Coastal walioweka kambi ya mwezi mmoja kisiwani
Pemba wamecheza mechi ya kirafiki na Polisi Morogoro ili kusindikiza tamasha
hilo.
Afisa habari wa Coastal Union, Oscar Assenga
amesema wagosi wa kaya wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
timu hiyo mpya ya ligi kuu msimu ujao.
Assenga alisema mabao ya Coastal Union yalifungwa
katika dakika ya 35 na Ramadhan Salum aliyesajiliwa kutokea Gor Mahia ya Kenya
na la pili likafungwa na Iker Bright Obina.
Baada ya mechi hiyo wachezaji wapya
walitambulishwa mbele ya mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego akiambatana na
mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Ahmed Aurora.
Picha za matukio ya tamasha hilo zitakujia muda wowote.
No comments:
Post a Comment