Warembo
wanaotarajia kushiriki katika shindano la Miss Tanzania 2014 wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika hifadhi ya taifa
Mikumi jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Kaimu
Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro, Apaikunda
Mungure, akiwagawia vipeperushi warembo wa shindano la Miss Tanzania
2014 walio tembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha
utalii wa ndani. Vipeperushi hivyo vina taarifa mbalimbali za hifadhi
hiyo ya taifa.
Kaimu
Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro, Apaikunda
Mungure akiendelea kugawa vipeperushi kwa warembo hao.
Mwongoza watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro, Benina Mwananzila akiwapa maelezo warembo
wa Miss Tanzania 2014 juu ya bwawa la viboko na mamba lililopo katika
hifadhi hiyo wakati warembo hao walipo tembelea hifadhi hiyo jana ikiwa
ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Warembo
wa Redd’s Miss Tanzania 2014 wakiwa katika Camp ya Mbuyu iliyopo katika
hifadhi ya taifa Mikumi jana walipotembelea hifadhi hiyo ikiwa ni
sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Picha na Mpigapicha wetu.
No comments:
Post a Comment