Mwenyekiti wa Kikundi cha Tumaini Saccos, akiowanesha namna sanduku
maalumu la kutunzia taarifa za kikundi chao linavyolindwa, wakati
maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania walipokwenda hivi karibuni kukagua
miradi mbalimbali ya wananchi wilayani Arumeru inayowezeshwa na Taasisi
ya ACE AFRIKA kwa ufadhili wa TBL.
Mwanachama wa Tumaini Saccos ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kikundi
hicho akionesha baadhi ya shughuli anazozifanya mbazo amewezeshwa na ACE
AFRICA chini ya ufadhili wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Maofisa wa
TBL walikwenda hivi karibuni kukagua miradi ya kikundi hicho.
Mkulima wa bustani ya ndizi na mboga za majani, Isaya Supuk wa kijiji
cha Olmotonyi, wilayani Arumeru, Arusha akiwaonesha maofisa wa Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) na ACE AFRICA namna shamba lake lilivyostawi
wakati maofisa hao wa TBL walipokwenda hivi karibuni kukagua shughuli
hizo zilizofadhiliwa na na kampuni hiyo.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi
akizungumza na Mkurugenzi wa ACE AFRICA (TANZANIA), Joanna Waddington
ofisini kwake Arusha, hivi karibuni kuhusu ufadhili wao unaowezeshwa na
taasisi hiyo kwa wananchi wa Arumeru katika shuguli mbalimbali za
maendeleo..
No comments:
Post a Comment