Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 27, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUELEKEA SIKUKUU YA EID-EL-FITR


Jeshi la Polisi Tanzania linapenda kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wote, vyama vya siasa, taasisi mbalimbali za serikali, madhehebu ya dini, asasi za kiraia na vyombo vya habari kwa ushirikiano wa dhati katika kusimamia masuala ya amani na usalama hapa nchini.

Tunapoelekea kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini na kusheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu umeonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu.

Jeshi la Polisi linapenda kuwaondoa hofu wananchi wote kuwa, limejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi kote nchini wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote, aidha,  tunapenda kuwatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara, kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.

Katika kuhakikisha usalama kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi.
Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya starehe, hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, yakiwemo maduka, hoteli na maeneo ya benki. Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza wale ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji endapo uhalifu unatokea.

Vilevile, wazazi wawe makini na watoto wao na hasa disko toto, ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.

Aidha wananchi wachukue tahadhari watokapo kwenye makazi yao wasiache nyumba wazi ama bila mtu na watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya bali watoe taarifa haraka kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu nao au kwa namba ya simu ifuatayo 0754 785557, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba - SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

ULTIMATE SECURITY YAJIKITA ZAIDI KIULINZI


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate security,Jacqui Bothma na Meneja wa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo Pambwe Maulid wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari mapya 12 na pikipiki 14 zitakazotumika kwaajili ya kutoa huduma mbalimbali katika jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate security,Jacqui Bothma(kushoto)akimsikiliza Meneja wa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo Pambwe Maulid,(hawapo pichani)akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa magari mapya 12 ya kampuni hiyo na pikipiki 14 zitakazotumika kwaajili ya kutoa huduma mbalimbali katika jamii.
Baadhi ya walinzi wa kampuni ya Ultimate Security ya jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye pikipiki mpya zilizonunuliwa na kampuni hiyo kwaajili ya matumatumizi ya huduma za ulinzi katika jamii,wakati wa uzinduzi wa magari mapya 12 ya kampuni hiyo na pikipiki 14.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Ultimate Security ya jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi rasmi wa magari mapya na pikipiki zilizonunuliwa na kampuni hiyo kwaajili ya matumitumizi ya huduma za ulinzi katika jamii.
Msafara wa magari mapya 12 ya kampuni ya Ultimate Security ya jijini Dar es Salaam,yakiongozwa na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo katika barabara ya Alhassan Mwinyi,tayari kwaajili ya matumatumizi ya huduma za ulinzi katika jamii.

BOB JUNIOR AINGILIA BIFU LA DIAMOND NA ALIKIBA, HAYA NDO MAZITO ALIYOFUNGUKA


Msanii na Producer anaetamba na Bolingo kwa sasa Bob Junior "Sharobaro" leo ameongelea ama kutoa ushauri kuhusu kutokuelewana kati ya wasanii wawili wa Bongo Fleva Ally Kiba na Diamond Platnumz, Amesema kuwa Ally Kiba ni Best Vocal na Best Artist in Bongo na Africa hivyo amemtaka Mdogo
Mdogo ambae kwa jina la wimbo yani Diamond kumuheshimu Ally Kiba, Pia ameendelea kwa kumwambia Ndagushima kwa jina la wimbo yani Ommy Dimpoz kwamba ugomvi huo haumuhusu hivyo asitafute kiki kupitia Beef hiyo. 


Nanukuu "BIFU  SIO KITU KIZURI UNAJUA ALIKIBA NI BEST VOCAL ANAJUA AKIFANYA CHO KUJIINUA SO UKIMYA WAKE USIKUFANYE WW KUMTUKANA KIIVYO NA KUMSEMA VIBAYA ATA WW #NGAGUSHIMA HILI BIFU WW ALIKUHUSU ACHA KUTAFUTA KIK KUPITIA BIFU ZA WATU ALIKIBA UR THE BEST AND MY BEST ARTIST IN BONGO AND AFRIKA SO WW #mdogomDOGO 
 ALIKBA ITS UR BROTHER MUHESHIMU BHANA

ENZOY DAWA YA NGUVU YA KIUME INARETA HESHIMATANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU ENZOY

DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI
ALLY WA YANGA BOMBA UHURU NA MSIMBAZI 0787230551 AU 0652755838
PIGA SIMU KWA MR.MKUNJE O713827689, 0755074505 , au 0719 541366
,0652755838 UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM


BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884
SHULE YA UHURU FIKA JENGO LA AZAM BAKHRESA ULIZA NGAEJE 0713873412
MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU  ULIZA MACHELLAH 0713470492
ENZOY INALETA HESHIMA
Photo: whatsapp 0713406938
whatsapp 0713406938

TANGAZO LA UTAFITI NA MGANGA WA TIBA ZA JADI TANZANIA

DR. CHIFU UWEZO
DR. CHIFU UWEZO MOTO WA RADI KUTOKA KIGOMA SASA YUPO DAR ES SALAAM MAENEO YA GONGOLAMBOTO
ANARUDISHA MALI ILIYOPOTEA KAMA GARI,MIFUGO UWANJA,SHAMBA ,NYUMBA ILIYO DHULUMIWA PESA ZILIZOPOTEA
ANAIFANYA BIASHARA YAKO INUNULIKE NA KUFANYIA MAOMBI YA KUKUBALIKA

ANAFANYA MAZINDIKO MBALIMBALI KAMA VILE NYUMBA SHAMBA MALI NA KADHA WA KAZA 

WANAOWAI KUFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA NA MIGUU INAYOWAKA MOTTO KUVIMBA MIGUU 

DAWA YA KUKUZA KIUNGO CHOCHOTE MWILINI MAKALIO ,UUME NA KUPUNGUZA MATITI TUMBO

DAWA ZA NGUVU ZA KIUMA AMBAZO ZINASAIDIA KUSHILIKI TENDO LA NDOA KIKAMILIFU PAMOJA NA DAWA ZA NGUVU ZA KIUME
YOTE YANAWEZEKANA KWA UWEZO WA MUNGU
WOTE MNAKARIBISHWA KWA DR,CHIFU UWEZO MOTO WA RADI KWA MAELEZO ZAIDI
PIGA SIMU NAMBA
0719272582
0688000893
0756095435
NB TIBA KWA WATOTO WADOGO NA WAZEE NI BURE KWA WATU WAZIMA MALIPO MPAKA MAFANIKIO YAONEKANE

SIMANZI ZAENDELEA KUTAWALA NDANI YA NYUMBA YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) MARA BAADA YA MSHIRIKI MWINGINE KUAGA SHINDANO


Majaji wa shindano la TMT wakimsikiliza kwa makini Mshiriki wa TMT, Mwanaafa Mwinzago (anayeonekana kwenye runinga mbele) wakati akijielezea kabla ya filamu fupi aliyoshiriki kuonyeshwa ili majaji waweze kutoa hukumu kwa washiriki wa kundi hilo
 Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) katikati wakiwasikiliza washiriki wa kundi la kwanza wanavyojielezea kabla ya filamu fupi waliyochezwa kuonyeshwa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wiki iliyopita
 Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiangalia filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) katika ukumbi wa makumbusho kabla ya kuanza kutoa hukumu kwa washiriki ni nani anatoka na nani anabaki.
Jaji Vyonne Cherry au Monalisa akitoa maoni kwa washiriki waliokuwa wameshiriki kwenye filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa TMT.
BOFYA HAPA KWA PICHA NA KUSOMA ZAIDI»

NSSF YAFUTURISHA WASTAAFU WAKE MKOA WA TANGAPrinciple Operation Officer wa NSSF, Joyce Mruma akigawa zawadi kwa wastaafu wa NSSF wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na shirika hilo. 
Ofisa Mwandamizi wa Operesheni wa NSSF, Lydia Ignace akitoa zawadi kwa wastaafu wa Shirika hilo waliohudhuria hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
Principle Operation Officer wa NSSF, Joyce Mruma akitoa zawadi kwa mstaafu wa NSSF, Bella Antao wakati wa hafla ya kufuturisha wastaafu wa Shirika hilo.

MWIGULU NCHEMBA ALIVYOLITEKA JIJI LA MWANZA


 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, akiwasili kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, kuhutubia mkutano wa hadhara, uliofanyika leo jioni. Katika Mkutano huo, Mwigulu amezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo, umuhimu wa wanasiasa na Watanzania kwa jumla kutolifanyia mzaha suala la mchakato wa Katiba mpya akivitaka vyama vya upinzani kuthamini zaidi vikao vya Bunge la Katiba ili kukamilisha mchakato huo kwa mazungumzo na mjadala uliojaa hekima badala ya kwenda mitaani kusumbua wananchi.

RAIS KIKWETE ATUNUKU WAHITIMU WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI KATIKA MAHAFALI YA KOZI YA PILI


 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe. Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. 
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika  mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka  nchi za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia na Zimbabwe.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.
Picha ya Pamoja.PICHA NA IKULU

KIPINDI CHA “MIMI NA TANZANIA” CHAVUKA MIPAKA YA TANZANIA, CHATUA JIJI LA WASHINGTON DC


IMG-20140725-WA0004
Pichani ni Mtangazaji anayeongoza Kipindi cha 'Mimi na Tanzania' Hoyce Temu aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 akiwa nje ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani mara baada ya kuwasili ambapo alimua kufunga safari kwa ajili ya kufanya mazungumzo maalum na Balozi wetu wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula.
IMG-20140725-WA0006
Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani.
IMG-20140725-WA0005
Hapa akiwa mapokezi ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani huku akisema ...Naipenda Tanzania yangu!
IMG-20140725-WA0003
Hoyce Temu akiangalia baadhi ya picha za Mabalozi 15 ambao tayari wameshaongoza Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani. wakiwemo Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, Mustafa Nyang'anyi na Balozi Ombeni Sefue pamoja Wanawake wawili ambao ni Mama Balozi Mwanaidi Maajar na Balozi wa sasa Mh. Liberata MulaMula.
IMG-20140725-WA0007
Mheshimiwa Balozi Liberata MulaMula ndani ya mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ofisini kwake jijini Washington DC, Marekani!
Mahojiano hayo ya moja kwa moja katika Balozi ya Tanzania nchini Marekani na Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula ambapo wameangazia masuala mbalimbali yakiwemo Utalii, kujitangaza katika miradi ya kimaendeleo na uwekezaji ,malalamiko ya watanzania waishio Marekani kuhusu uraia, kwa mengineyo mengi usikose kuangalia Channel Ten wiki ijayo Jumapili saa moja na nusu usiku kilicho bora kabisa.

FUN CITY YAWAKARIBISHA KATIKA EID

Funcity
Funcity

FUNCITY

EID
Funanza - 5
  • Acrobatic & Circus
  • Fun Rides and Water Sports
  • Comedy Show & Live Entertainment
  • Hands on Sports competition
  • Special Eid Lunch
  • Face Painting
  • Prizes & Complimentary Passes
        and a lot more fun!
Burudika Eid na FUNCITY....burudisho la wote
123Tanzania E-Shots

30,000+ Subscribers all over the Tanzania. 123Tanzania.com is the largest B2B online directory of Tanzania with more than 15,000 monthly visitors

Contact 123tanzania.com: English or Kiswahili +255 658 786 235, +255 773 858 090, +255 22 213 3039

Saturday, July 26, 2014

MFUKO WA PESHENI KWA WATUMISHI WA UMMA 'PSPF' WATOA SEMINA KWA WASANII WA BONGO MOVIE

   Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu kushoto akisalimiana na msanii Rose Ndauka wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko huo kwa ajili ya kutoa elimu na kujiunga katika mfuko huo Dar es salaam juzi kulia ni msanii Ester Kiama picha na mpiga picha wetu
 Baadhi ya wasanii wakijadiliana jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na mfuko wa wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF'
  Mwigizaji na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mengere a.k.a 'Steve Nyerere' kushoto akizungumza wakati wa semina kwa ajili ya wasanii iliyoandaliwa na mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' juzi makao makuu ya mfuko huo Dar es salaam juzi picha na mpiga picha wetu
Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu kushoto akizungumza na wasanii Rose Ndauka wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko huo kwa ajili ya kutoa elimu na kujiunga katika mfuko huo Dar es salaam juzi kulia ni msanii Ester Kiama picha na mpiga picha wetu

 Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu wa pili kushoto akizungumza na wasanii baada ya kufungua semina kwa ajili ya wasanii mbalimbali
 Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu kushoto akisalimiana na kocha wa timu ya simba msimu uliopita Jamuhuri Kiweru
wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko huo kwa ajili ya kutoa elimu na kujiunga katika mfuko huo Dar es salaam juzi katikati ni Afisa Masoko wa mfuko huo Rahma Ngassa picha na mpigapicha wetu
BAADHI YA WATU WALIOHUDHULIA SEMINA HIYO

Friday, July 25, 2014

CHAMA CHA NGUMI ZA KULIPWA TPBC CHATOA MAFUNZO KWA MAREFARII

Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' kushoto akiwaelekeza baadhi ya marefarii waliojitokeza katika mafunzo hayo yaliyo andaliwa na chama cha ngumi za kulipwa TPBC yaliyoanza Ilala CCM Dar es salaam juzi na kumalizika jumamosi  hii picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' kulia akisisitiza jambo kwa wakati wa mafunzo hayo uku marefarii waliojitokeza wakimsikiliza kwa makini kutoka kushoto ni Kondo Nassoro, Sako Mtlya na Buchato Michael picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' akitoa maelekezo kwa mabondia na marefarii kabla ya kupigana wakati wa mafunzo kwa vitendo ya urefarii wa mchezo huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

BAADHI YA MAREFARII WALIOSHILIKI KATIKA KOZI HIYO KUTOKA KUSHOTO NI BUCHATO MICHAEL,PEMBE NDAVA,HAMISI KIMANGA,RAJABU MHAMILA 'SUPER D' ALLY BAKARI,Ayubu Tezikoma NA SAKO MTLYA

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA LEO


  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kasimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwela ngao kwenye mnara wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa  yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo. Wengine ni  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Waziri Mkuu Mzengo Pinda leo Julai 25, 2014
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Frederick Sumaye  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo.
Wengine toka kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Mkuu wa Tanzania,  Mhe Mohamed Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar  Mhe omar  Othman makungu leo Julai 25, 2014
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiamkiana na wazee wa Tanzania Legion waliopigana katika vitra kuu ya dunia ya pili  waliohudhuria  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014 PICHA NA IKULU
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...