Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, January 31, 2014

SUPER D AMPONGEZA BONDIA MUSSA MCHOMANGA NA KUMZAWADIA


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi clip bandeji na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa bondia Mussa Mchopanga baada ya kumdunda Anton Idoa kwa K,o ya raundi ya pili bondia huyo ndie bingwa kwa sasa wa mkoa wa Dar ers salaam na anajiandaa na mashindano ya Majiji yatakayofanyika katikati ya mwaka huu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Anton Idoa akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mussa mchopanga wakati wa mashindano ya Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Panandi panandi Ilala Mchopanga alishinda raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Anton Idoa kushoto akirusha konde ambalo alijareta madhala kwa mpinzani wake ambae anamwangalia Mussa Mchopanga wakati wa Mashindano ya Mkoa wa Dar es salaam Mchopanga alishinda kwa K,O ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Kocha Mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akimwinua mkono juu bondia Mussa Mchopanga baada ya kumvalisha medali ya Dhaabu baada ya kuibuka mshindi wa mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi clip bandeji na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa bondia Mussa Mchopanga baada ya kumdunda Anton Idoa kwa K,o ya raundi ya pili bondia huyo ndie bingwa kwa sasa wa mkoa wa Dar ers salaam na anajiandaa na mashindano ya Majiji yatakayofanyika katikati ya mwaka huu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi cheti kwa bondia Mohamed Chibumbuli mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi cheti kwa bondia Mohamed Chibumbuli mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimvisha medali ya dhaabu bondia Mohamed Chibumbuli mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimvisha medali ya Fedha bondia Abdul Rashidi  mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Thursday, January 30, 2014

KAMATI YA PAC YAFANYA UKAGUZI VITABU VYA CHENJI YA RADA DAR


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, (CHADEMA), Zitto Kabwe, akiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014, akikagua vitabu vya ziada. Kamati ya bunge ya PAC, ilifanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini kama vitabu vilivyonunuliwa kutokana na chenji ya rada vimekwishagawiwa kwenye shule mbalimbali kama ilivyoahidi serikali. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kamati yake ilikuta vitabu hivyo vikitumiwa na wanafunzi.

Zitto akizungumza na wanafunzi
Wanafunzi wakipiga makofi, wakati mwenyekiti huyo akizungumza nao
Wanafunzi wakisikiliza maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, kwenye shule ya msingi Bunge katikati ya jiji la Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014.Picha na K-Vis Blog.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MAWAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, SAYANSI ELIMU IKULU DAR.


UNIC yaendelea kutoa mafunzo ya mateso ya kambi za wayahudi

DSC_0014
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.
Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.
“Ni muhimu kutoa mafunzo kwa vijana wakitanzania wa shule za msingi na sekondari ili wajue kwamba tofauti za rangi na za kidini hazina nafasi ya kutugawa kama binadamu,” amesema Nkhoma.
DSC_0005
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Diamond na Mlezi wao wakimsikiliza Bi. Ledama (hayupo pichani).
DSC_0044
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto.
Alisisitiza kwamba mauaji na mateso ya Auschwitz yalipoteza mamilioni ya watu wasio na hatia na mafunzo haya yanaonyesha chuki na ubaguzi dhidi ya wayahudi na chuki za aina nyingine yoyote hazina nafasi katika ulimwengu wa leo.
Nkhoma amesema kwamba binadamu wote ni sawa na tofauti za kipato au dini au rangi haziwezi tena kujenga chuki dhidi ya binadamu wengine kwa sababu wote kama binadamu tuna haki sawa mbele za mungu.
DSC_0051
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond jijini Dar es Salaam, wakifuatilia sinema maalum ya mauaji ya kambi za mateso ya wayahudi mwaka 1933.
Wakati huo huo, ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto amesema aliona makambi ambako wayahudi, waroma, wasinti, mashoga, wafungwa wa kivita na watu wenye ulemavu walitumia siku za mwisho katika hali ya kinyama.
“Umoja wa Mataifa ulianzishwa kuzuia kila aina hii ya fazaa kutokea tena, lakini bado misiba kuanzia Cambodia hadi Rwanda mpaka Srebrenica inaonyesha kuwa sumu ya mauaji ya kimbari bado inatiririka,” ilisema taarifa hiyo.
DSC_0082
Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond wakisoma baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa.

VYAMA VYA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI VYAUNGANA KUWAKUTANISHA MABONDIA JUMAMOSI

Vyama vya ngumi za kulipwa nchini  vimekubali  kuungana na wenzao TPBO kushiriki mkutano wa mapromota wa ngumi na mabondia wote wa Tanzania. Mkutano huo unaotarajiwa  kufanyika katika ukumbi wa vijana Kinondoni, siku ya jumamosi tarehe 1/2/2014 kuanzia  saa nne asubuhi. Mkutano huo ulioitishwa na TPBO chini ya udhamini wa KITWE GENERAL TRADERS ukiwa na lengo la kuweka mikakati ya sasa na ya baadae kwa ajili ya kuinua ngumi za hapa nchini,sanjali na kutambulikana kwa mapromota na mabondia wenyewe kwa kutengenezewa vyeti maalum na vitambulisho, vitakavyowafanya watambulike katika jamii ya wanamasumbwi wa hapa Tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi yetu,hizo ni sehemu ya mada zitakazozungumzwa.
Ibrahim kamwe akizungumza na vyombo vya habari ,alisema ‘Mkutano huo ambao utawahusisha mapromota wote ,pamoja na viongozi wa vyama vya ngumi za kulipwa,makocha na mabondia wote wa ngumi za kulipwa, haijalishi wewe ni nani ili mradi ni mwalimu wa ngumi, mratibu wa ngumi au bondia ni vema ukafika katika mkutano huo ambao ni mara ya kwanza kufanyika  katika historia ya ngumi za kulipwa kuwakutanisha kwa pamoja waratibu, viongozi na mabondia wa nchi nzima kwa pamoja, pia mkutano huo utaendana na mapromota kupewa vyeti  na kurekebisha usajili wa mabondia ambao usajili wao haujakaa sawa.


 

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU DAR


 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri na Manaibu Waziri waliokuwa wakiapisha Ikulu Dar es Salaam, leo wakati alipokuwa akiwasili katika hafla hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha George Boniface Tuguluvala Simbachawene, kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Saning’o Telele, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakia katika picha ya pamoja na Waziri na Manaibu Waziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.

LG yazindua aina ya OLED TV nchini Tanzania


Ofisa Mauzo wa Kampuni ya LG Bw, Valerian Banda akionesha mawani kwa ajili ya kuangalia TV ya Oled ambayo kwa mara ya kwanza imeingizwa nchini sasa zinapatikana katika maduka yote ya LG
Dar es Salaam, tarehe 29 January 2014 – LG imezindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania, TV aina ya OLED inayojikunja ni mwanzo wa burudani ndani ya nyumba. Aina yake ya kujikunja ambayo inaitwa IMAX inatupa uzoefu wa hali ya juu pamoja na kuangalia kwa starehe kubwa.
TV hii mpya aina ya OLED kutoka LG ikiwa na teknolojia ya rangi nne, ambayo kwa mujibu wa kampuni inaongeza pikseli nyeupe kwa rangi nyekundu, kijani na blu kwa mtazamo bora. Itakuwa na screen nyembamba aina ya OLED ambayo ukubwa wake ni 4.3mm. Pamoja na stendi yake ambayo ina vipimo ifuatavyo 1227x799x192mm na uzito wa kilo 17.2.  
 TV aina ya OLED LG namba 55EA9800 inakuja na idadi ya chaguo ya kuunganisha ambayo ni HDMI port (x4), port ya kusikiliza muziki ( 3.5mm), RF, AV ( composite), port ya muziki, USB 2.0 (x2), USB 3.0 na LAN port.”
TV hii pia ina kitako ambacho ni wazi kama kioo ambacho TV huwa haionekani kama imeungana nacho na TV huonekana kama inaning’inia hewani. Pia TV hii imewezeshwa kuwa na muonekano wa spika tano kwenye kitako chenye LG 55EA9800 zenye uwezo waku toa sauti ya watti 40.
Bwana Rajesh Darji, wa Garnet Star Ltd Distributor wa LG Home Entertainment Products amesema“ Hii TV aina ya OLED inapatikana katika maduka makubwa ya LG na wakala wake.
Hii itampa mteja  uonaji mzuri isiyokuwa na mwisho. Burudani ya nyumbani imejazwa na mabadiliko yanayo endelea kila siku na sisi kama kampuni ya LG ni kazi yetu kuwa letea bidhaa inayoendana na wakati huu”
Mtengenezaji kutoka Korea ya Kusini amekaririwa akisema kuwa utendaji waLG 55EA9800 una kasi mara mia zaidi ya TV zingine aina ya LED/LCD, ambayo inaweza kupunguza mwanga wa picha zinazo jionesha kwa kasi katika kioo cha TV
Kampuni ya LG imeongeza‘rimoti ya ajabu’yenye uwezo wa kupokea sauti na ishara na mchanganyiko wa mambo mbali mbali.

Wednesday, January 29, 2014

WAKAMATWA COCO BEACH WAKIFANYA NGONO




NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.

Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa…

NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.

Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi mmoja na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa).

BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ
Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana, aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.

Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo.
Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote kwa pamoja.
Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.

ALIKWENDA KUKUMBUSHIA ENZI ZAKE
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo.
Alijitetea kuwa mume wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’ aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini.
Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.

BINTI WA KIGOGO
Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini akiwa kwenye kundi la makahaba.
Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.

MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE

MGAMBO MANISPAA YA IRINGA WAWAKIMBIZA WANAUJENGA MILIMANI


Mgambo  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakikisambaratisha kibanda  kilichojengwa katika mlima wa Nzizi la Ng'ombe kama  sehemu ya utekelezaji wa agizo la mstahiki meya  wa Manispaa  hiyo Aman Mwamwindi na mkurugenzi wake Terresia Mahongo kwa  kutaka  wale  wote wanaovamia milima kwa ujenzi kuvunjiwa nyumba zao 
Baadhi ya  nyumba  zilizojengwa milima bila  kibali na kuvunjwa 
Afisa mtendaji  wa kata ya Mwangata Bw  Mlole   akionyesha nyumba  iliyovunjwa baada ya  kujengwa mlimani 
Mgambo  wakikusanya mabati na kutatuma korongoni 
Hawa nao  walikutwa eneo  hilo la Zizi wakijenga bila  kibali ,wimbi la  wananchi wa mji wa Iringa kuvamia milima na kujenga  limeendelea kuwa kubwa pamoja na  Halmashauri hiyo  kupiga marufuku ujenzi usio na vibali katika milima

CHOPA YA DR SLAA YAKWAMA IRINGA UWANJA WA NDEGE YAKOSA WESE (MAFUTA)


 mmoja  kati ya  Helkopta  za Chadema ikiwa  hewani
Hii  ndio  Helkopta  aliyokuwa akiitumia  katibu mkuu wa Chadema Dr Slaa katika mikutano yake nyanda za juu  kusini ikiwa  imetua katika  uwanja  wa mikutano wa Mwembetogwa na baada ya hapo  ilipelekwa  kuegeshwa  uwanja wa Ndege  Nduli  kutokana na kuishiwa  mafuta  hivyo kulazimika  baadhi ya maeneo  kushindwa kwenda kwa usafiri  huo na badala yake viongozi wake  kutumia magari .

Kuna haja  ya  kuwepo kwa  kisima cha uuzaji wa mafuta ya Ndege katika uwanja  wa Ndege Nduli Iringa ili  kuepusha usumbufu  wa Ndege kwenda  kujaza ama kununua mafuta  Dodoma
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...