Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 13, 2014

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII LAZARO NYALANDU AAGIZA KUMALIZWA KWA MIGOGORO YA MIPAKA BAINA YA WANANCHI; HIFADHI ZA TARANGIRE NA PORI LA AKIBA LA MKUNGUNERO.


Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Manyara na Dodoma wakati wa kikao maalum cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Elaston Mbwilo akisitiza jambo wakati wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi
  1. Sehemu wa wajumbe waliokutana katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Kutoka kulia: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwilo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakifuatilia mada.
  1. Kutoka kulia: Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Profesa Alexander Songorwa na KatibuTawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Serikali ameagiza kumalizwa kwa migogoro ya mipaka baina ya Hifadhi ya Tarangire, Pori la Akiba la Mkungunero na wananchi iliyodumu kwa  muda wa takribani miaka kumi hadi sasa. 
Nyalandu amewataka wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi hizo kuacha kuvamia maeneo yaliyotengwa kisheria kwani kwa kufanya hivyo ni kuleta migogoro isiyo ya lazima.
Mhe. Nyalandu alikuwa akiongea katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Manayara na Dodoma wilayani Babati mkoani Manyara zilizokutana kwa ajili ya kujadili suluhu ya migogoro hiyo. 
Aliongeza kusema kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro hiyo kwa kuishirikisha jamii kwa upana zaidi huku akisisitiza kwamba Serikali itaendelea kusimamia na kutekeleza Sheria ya Uhifadhi bila kumuonea mwananchi yoyote na kwa kuzingatia haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...