Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan akiwasalimu wachezaji wa timu ya Kinondoni |
Mbunge wa Kinondoni akiwasalimu wachezaji wa Temeke |
Mbunge wa Temeke Abass Mtemvu akiteta jambo na wachezaji wa Temeke wakati wa mapumziko |
Idd Azan naye hapa anajitahidi kuteta na wachezaji wa Kinondoni wakati wa mapumziko baada ya kuona jahazi zinazama |
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akimkabidhi Katibu wa Chaneta, Anna Kibira, pesa taslimu 1,000,000 |
Baadhi ya wadau waliokuwepo |
TIMU za mchezo wa pete ya mkoa wa Temeke na Morogoro zimeingia fainali ya
mashindano ya Taifa Cup, baada ya kushinda michezo yao leo iliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Temeke ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo walianza
kuliandama lango la Kinondoni tangu robo ya kwanza ya mchezo kwani walikwenda
mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 14 na Kinondoni wakiwa na mabao 9.
Kama vile haitoshi huku kila timu ikihamasisha na mbunge
wake, Temeke wakiwa na Abbas Mtemvu huku Kinondoni wakiwa na Idd Azan
waliendelea kuoneshana ushindani lakini Temeke waling’aa zaidi baada ya
kuifunga Kinondoni mabao 16 kwa 9.
Kwenye robo ya tatu Kinondoni walipotea kabisa na kujikuta
wakifungwa mabao 17 kwa 5 na robo ya nne ya kukamilisha mchezo Kinondoni
walizidi kuelemewa baada ya kupokea kipigo cha mabao 19 kwa 10.
Kinondoni hawatamsahau GS wa Temeke Mwanaidi Hassan kwani
ndiye alikuwa mwiba mchengu kwa kutumbukiza mabao mengi katika mchezo wao.
Nusu fainali ya pili ilizikutanisha timu za Morogoro na
Katavi ambapo Morogoro ndiye atakayecheza fainali na Temeke baada ya kuifunga Katavi mabao 50 kwa 29.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mbunge wa Temeke, Abbas
Mtemvu alisema kuwa Temeke wanafanya vizuri na watatetea ubingwa wake kutokana
na maandalizi mazuri walioyafanya huku mbunge wa Kinondoni, Idd Azan akizitaka
halmashauri kusaidia timu zinazowakilisha mikoa kwani zina mafungu maalum kwa
ajili ya michezo.
Naye Katibu wa Chama cha Netbali (CHANETA) Anna Kibira alimpongeza
na kumshukuru Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kwa jinsi alivyojitoa kukisaidia
Chama cha Netbali na kuomba wadau
wengine kujitokeza kuinua mchezo huo ambao unatoa ajira kwa vijana.
‘Namshukuru Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu kwani leo
ametimiza ahadi yake ya kukisaidia CHANETA 1,000,000 ambazo amekabidhi mbele
yenu hivyo naomba watu wengune na makapuni yasaidie mchezo huu kwani unatoa
ajira kwa vijana”, alisema Kibira.
No comments:
Post a Comment