Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, January 10, 2014

ASKARI POLISI NA ASKARI MAGEREZA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA MBEYA.


Ulinzi ukiimarishwa Baada ya watuhumiwa wa ujambazi kufikishwa mahakamani
Mbele ni mshitakiwa wa nne Mbaruku Hamis akiingia mahakamani
Kutoka kushoto ni mshitakiwa wa pili Elinanzi Eliabu Mshana, Mshtakiwa wa nne Mbaruku Hamis, Mshita kiwa wa tatu Juma Mussa ambaye aliyekuwa Askari Magereza kwa Cheo cha Sajini , Anaefuatia ni Mshtakiwa wa kwanza PC James aliyekuwa Askari Polisi Wilaya ya Mbeya, na wa mwisho ni Mshitakiwa wa Tano Amri Kihenya .
Wa kwanza kushoto aliye vaa shati la Draft ni Dereva Ezekia Matatila (34) pamoja na wasikilizaji
Moja ya Gari lililotumika kufanya uharifu wa unyang'anyi wa kutumia silaha 
Washitakiwa wanne kati ya watano kutoka kushoto juu hadi wa nne wakiwa wanatoka mahakamani chini ya ulinzi mkali.
Mwenye Jaketi la Njano ndiye Mshitakiwa namba moja PC James 
Katikati ni Mke wa mshitakiwa wa tatu ambaye ni Askari Magereza Sajini Juma Mussa, Hata hivyo mwanamke huyo alizirai mahakamani wakati mumewe akiwa kizimbani.

**********************************

ASKARI  wawili wa jeshi la Polisi na Magereza pamoja na watu watatu ambao ni raia wa   kawaida wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya wakituhumiwa kwa  ujambazi wa kutumia silaha. Watuhumiwa  hao watano kwa pamoja walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya  Wilaya ya Mbeya, Michael Mteite wakituhumiwa kwa kosa moja la unyang’anyi wa  kutumia Silaha kinyume cha Sheria kifungu cha 287 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. 

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni  Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba F8302 wa  Wilaya ya Mbeya ambaye kabla ya kufikishwa mahakamani alivuliwa Uaskari baada ya kuhukumiwa kijeshi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...