Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, January 22, 2014

MIAKA 25 YA NDOA YA CHARLES & BETTY MKWASA


Wana Silver Jubilee, Betty Mkwasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma na mumewe Charles Boniface Mkwasa 'Master' Kocha msaidizi wa Yanga, wakionesha hati maalum ya ndoa kutoka kwa Papa Francis. Hati hiyo ya heshima hutolewa na Papa kwa wanandoa waliotimiza miaka 25 ya ndoa yao. Mkwasa na mkewe walitimiza miaka 25 ya ndoa yao Januari 14 mwaka huu na jana Januari 18 kuafanya misa maalum ya kubariki ndoa yao na kurejea viapo vyao vya ndoa.
Production by: MD Digital Company +255 7170023/+255 373999
Haya ndio matunda ya ndoa ya Bwana na Bibi Mkwasa
Waziri wanchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, Willium Lukuvi na mkewe nao walikuwepo. Katikati ni Mama mzazi wa Betty Mkwasa.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Betty Mkwasa akimkabidhi zawadi ya jezi namba 8 ya timu ya Yanga, Mumewe ambaye pia ni kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa wakati wa tafrija ya Jubilei yao ya ndoa ya miaka 25 juzi Dar es Salaam.
Wakulima na wananchi kutoka Bahi ambako Mheshimiwa Betty Mkwasa anafanyia kazi walileta kuku wa kienyeji na mafuta ya alizeti lita zaidi ya 30, Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, bata Mzinga na nafaka za mahindi na mchele kwa maharusi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...