Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, January 4, 2014

MAMA AJIFUNGUA WATOTO WANNE MKOANI MBEYA , AOMBA MSAADA KWA WATANZANIA






Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.
Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo.
kikosi cha blog ya Mbeya yetu  Kikiongozwa na Joseph Mwaisango ambacho kilifika kumjulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kidogo wa nguo za watoto sabuni  chupa na dishi  hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake.
Katibu msaidizi wa hospitali ya  Rufaa Mbeya Mwansasu akipokea msaada huo kwa niaba ya mzazi

KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida Mwanamke mmoja, Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri. Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa
anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...