Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 29, 2016

MAZOEZI MAKALI YANAENDELEA KATIKA KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM KARIAKOO

Mabondia Faraji Sayuni kushoto na Hassani Kiwale wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Kariakoo mabondia wote hawo watapanda uringoni agost 8 katika ukumbi wa kobelo pub manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

 Bondia Hassani Kiwale kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Faraji Sayuni wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika katika kambi ya Super DCoach Uhuru GYM Kariakoo Dar es salaam mabonda hawo watapanda uringoni Agost 8 kuwakabili wapinzani wao katika ukumbi wa kobelo pub manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwasimamia mazoezi mabondia Faraji Sayuni kushoto na Hassani Kiwale wakati ya mazoezi yao yanayoendelea katika kambi ya Super D coach Uhuru GYM Kariakoo Dar Es Salaam 

Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa ubingwa wa taifa wa kg 57 utagombaniwa na mabondia Kais Rashidi Na Faraji Sayuni siku ya Agost 8 katika ukumbi wa Kobelo Pub Manzese Dar Es Salaam  

mpambano uho wa raundi kumi za ubingwa umeratibiwa na Promot Miraji Uliza ambapo kutakuwa na mapambano mengine mbalimbali ya mchezo wa masumbwi nchini

mabondia wengine watakaopanda siku hiyo ni Abdallah Pazi atakaezipiga na Said Mkone wakati godrack Mrema atakumbana na Hassani Kiwale wakati Omari Uliza atazipiga na Bruno Fadhili na Said Jelemi atamkabili Azizi Kondo na Saleh Mkalekwa atacheza na Salum Ngula na Azizi Uliza atacheza na Mohamed Matimbwa

pamoja na mapambano mengine mengi

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

MISS TANGA KUFANYIKA TANGA BEACH RESORT

 Warembo wanaowania Taji la Mrembo wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016) wakiwa kwenye pozi katika hotel ya Tanga Beach Resort kutakapofanyika shindano hilo Ijumaa Julai 29.2016.

Warembo hao wakiwa kwenye picha ya pozi

Warembo wanaowania Taji la Urembo Mkoa wa Tanga(Miss Tanga 2016) ambalo linaandaliwa na Kituo cha Radio cha TK FM cha Mjini Tanga kwa kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wakiwa kwenye picha ya mapozi

Mratibu wa Shindano ya Miss Tanga 2016,Mboni Muya akizungumza na waandishi wa Habari leo kuhusiana na maandalizi ya kuelekea shindano hilo

Baadhi ya Warembo wakimsikiliza Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini Sinza,Beny Kisaka alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuitembelea kambi ya warembo hao wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Nassoro Makau

Warembo hao wakimsikiliza Mratibu wa Shindano ya Miss Sinza 2016 ambaye aliitembelea kambi hiyo leo

 Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini,Benny Kisaka akitoa nasaha kwa warembo wanaotarajiwa kushiriki kinyang'anyiro cha kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016 )itakayofanyika Ijumaa kesho  kwenye Ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort.
 Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini,Benny Kisaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga Ijumaa

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MABONDIA KUTOKA KWA SUPER D COACH UHURU GYM

MABONDIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA MAZOEZI YAO YANAYOFANYIKA KWA SUPER D COACH UHURU GYM KARIAKOO KUTOKA KUSHOTO NI HASSANI KIWALE 'MORO BEST' KG 51 MOHAMED KISEA KG 54 FARAJI SAYUNI KG 56 IDDI MKWELA KG 61 VICENT MBILINYI KG 63 GESPER MSEVENI KG 66 NA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
BAADHI YA MABONDIA WALIOPO KATIKA KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM
BAADHI YA MABONDIA WALIOPO KATIKA KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM
KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D AKIWA NA  MABONDIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA MAZOEZI YAO YANAYOFANYIKA KWA SUPER D COACH UHURU GYM KUTOKA KUSHOTO NI HASSANI KIWALE 'MORO BEST' KG 51 MOHAMED KISEA KG 54 FARAJI SAYUNI KG 56 IDDI MKWELA KG 61 VICENT MBILINYI KG 63 GESPER MSEVENI KG 66

KOCHA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KUSHOTO NI FARAJI SAYUNI NA HASSANI KIWALE
KOCHA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KUSHOTO NI FARAJI SAYUNI NA HASSANI KIWALE

MRADI WA HARAMBEE NI MKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHOLE, MAFIA - PWANI

Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha Chole ikiwa ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta mkanganyiko hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya kale kinyume cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile linachafua sura ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. --- Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog - CHOLE, MAFIA. Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia - Pwani wameusifia mradi wa Harambee unaowapatia elimu watoto wao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog iliyoweka kambi kijijini hapo kujionea hali halisi ya kisiwa hicho, wananchi hao walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi wa wanachi kwa vile ni mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao amekuwepo mwekezaji kijijini hapo. Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman alisema mpaka sasa zaidi ya Sh. milioni 500 zimetumika kugharimia ada na mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni wa kijiji cha Chole, kupitia mradi huo. Aliongeza kuwa pesa hiyo imeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi wapatao 300.
Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Chole (kulia) ambaye alianza kazi yake 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Pembeni ni mwenyekiti wa sasa Shehari Ahmadi. Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee.  Mkazi wa Chole, Bw. Johari Rajabu Fadhil ambaye ndiye mmoja ya waasisi waliompokea mwekezaji, na aliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo ya kufundisha watoto ya miaka 2.
 Mkazi wa kwanza wa kijiji cha Chole wilayani Mafia kijiji cha Chole Mjini kupata digrii ya chuo kikuu, Zubeda Bhai akiwaelezea waandishi wa habari abato Kasika na Florence Mugarula waliotembelea eneo hilo la kihistoria jinsi ambavyo taasisi ya Chole Mjini Conservation and Development ilivyomsaidia gharama zote za kupata elimu ya juu. --- Alisema kuwa miaka ya nyuma wakazi wa Chole hawakuwa na mwamko wa elimu, lakini baadaye wakapata mwekezaji ambaye amechangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwafanya wakazi wa kisiwa hicho kuwa nma mwamko wa elimu. "Tuna mwekezaji ambaye ni kampuni ya Chole Conservation & Development inayosimamia na kutunza magofu ya Kijerumani, ametusaidia sana kutuamsha na sasa hapa Chole kuna mwamko mkubwa wa elimu," alisema Kingi. Alisema kuwa mwekezaji huyo aliwahamasisha kuanzia kamati hiyo ndipo ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba ukaanza kuongezeka kuanzia mwaka 2007 na umekuwa ukizidi kupanda kadri miaka inavyokwenda.
 Wanafunzi wa Chekechea wakifundishwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wanaonufaika na mfuko wa maendeleo wa Harambee. wakiwa pamoja na mkurugenzi wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development Bi. Anne K. de Villiers.
Moja ya usafiri wa boti unaotumika kuwavusha wakazi wa Chole kwenda Mafia Mjini.
Wageni waliofika kutembelea kisiwa cha Chole kujionea majumba ya kizamani yenye histori za mababu zetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman akielezea maendeleo ya kijiji cha Chole katika upande wa elimu akiwa na  katibu wa kamati hiyo Mohamed Kingi (kulia).

Monday, July 25, 2016

MABONDIA WA KIKE KUPANDA URINGONI AGOST 7 UWANJA WA TAIFA KUWASINDIKIZA GALILE NA KALAMA

Promota wa mchezo w masumbwi nchini  Haruna Mussa 'Dippo' katikati akizungumza na mashabiki wa mchezo wa ngumi za kulipwa wakati alipowatambulisha kupigana kwa mabondia wa kike Halima Bandola na Joyce Awino watakao oneshana umwamwamba Agost 7 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha SUPER D BOXING NEWS

Promota wa mchezo w masumbwi nchini  Haruna Mussa katikati akiwainua juu mabondia mbele ya mashabiki wa mchezo wa ngumi za kulipwa wakati alipowatambulisha kupigana kwa mabondia wa kike Halima Bandola na Joyce Awino watakao oneshana umwamwamba Agost 7 katika uwanja wa ndani wa  Taifa Picha SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA wa kike katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Halima Bandola na Joyce Awino watapanda uringoni Agost 7 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa

akizungumza na mashabikiwa mchezo wa masumbwi wishoni mwa wiki iliyopita promota wa mpambano uho Haruna Mussa 'Dippo'

amesema ameamua kuwa promoto watoto wa kike kwa ajili ya kuhamasisa wasichana kuupenda na kuucheza mchezo wa masumbwi kwani kwa sasa michezo ni ajira kwa vijana

aliongeza kwa kusema katika mpambano uho kutakuwa na mpambano wa kukata na shoka mabondia Kalama Nyilawila atavaana na Selemani Galile mpambano wa raundi kumi katika uzito wa kg 72

wakati mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Meshack Mwankemwa kutoka Mbeya atakumbana na Selemani Zugo mpambano wa ubingwa wa KG 66 raundi kumi   
 Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

DVD MPYA KABISA ZA MASUMBWI SASA ZINAPATIKANA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI

DVD MPYA KABISA ZA MASUMBWI SASA ZINAPATIKANA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.burudan.blogspot.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

RAIS DK. MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA SIKU YA MASHUJAA KITAIFA MJINI DODOMA

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Sime katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016. PICHA ZOTE/IKULU
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Ngao katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma  Julai 25, 2016.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela baada ya kuongea na wananchi kwenye Madhimisho ya Siku ya Mashuja.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...