Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Nchini Kenya, SJAK, Mbais Criss, akimkabidhi zawadi ya
Kombe la mchezaji bora Nahodha wa timu ya TASWA QUEENS, Lightness
Sirikwa Mayeye, baada ya kutangazwa mchezaji bora aliyejituma katika
mchezo wao dhidi ya timu ya SJAK ya Kenya.
Timu hizo zilizoshiriki katika Bonanza
maalumu la Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani,
lililofanyika kwenye Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai
9, 2016, zilitoka sare ya 0-0 katika muda wa kawaida na kupigiana
penati ambapo Taswa Queens waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 4-3.
Picha na
Mafoto Blog
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Nchini Kenya, SJAK, Mbais Criss, akimkabidhi Kombe la
ushindi Kipa wa timu ya TASWA QUEENS, Somoe Ng'itu, baada ya timu hiyo
kuifunga timu ya SJAK ya Kenya kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu
hizo kutoka sare ya 0-0 katika muda wa kawaida.
Timu hizo zilishiriki kwa pamoja katika
Bonanza maalumu la Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani,
lililofanyika kwenye Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai
9, 2016.
Kiungo
wa timu ya Taswa Queens, Ester Zelamula
(kulia) akimtoka mchezaji wa Sjak ya Kenya, Mercy Njue, wakati wa mchezo wa kirafiki katika
Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, uliochezwa kwenye Uwanja wa
Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016. Katikati ni Lightness Sirikwa wa Taswa Queens akijiandaa kutoa msaada.
Kiungo wa timu ya Taswa Queens, Ester
Zelamula (kulia) akimtoka mchezaji wa Sjak ya Kenya, Mercy Njue,
(katikati) Kushoto ni Lightness Sirikwa wa Taswa Queens akijiandaa kutoa
msaada.
Zelamula akiambaa na mpira baada ya mtoka Mercy Njue..
Winga wa Taswa Queens, Angela Msangi
(kulia) akipiga shuti huku beki wa Sjak ya Kenya, Rebecca Magoma,
akijaribu kumdhibiti bila mafanikio.
Lightness (kulia) akichuana kuwania mpira na Mercy.....
Kipa wa Tswa Queens, Somoe Ng'itu akituliza mpira wakati wa mechi hiyo
Lightness akiambaa na mpira.....
Mtanange wa Taswa Fc dhidi ya Sjak ya Kenya ukiendelea. Katika mchezo huo Sjak waliibuka na ushindi.
Mshike mshike langoni mwa Sjak....
Julius Kihampa (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Sjak.......
Khadija Kalili wa Taswa Queens (katikati) akimdhibiti Eveline wa Sjak....
Angela Msangi akipiga shuti..........
Angela Msangi akichuana kuwania mpira na beki wa Sjak Rebecca Magoma
Ester Zeamula akifunga penati......
Kipa wa Taswa Queens Somoe Ng'itu akiokoa penati ya Eveline....
Kipa wa Taswa akibebwa juu kwa furaha baada ya kuokoa penati moja iliyowawezesha kuibuka kidedea.
Picha ya pamoja kabla ya kuanza mechi hizo..
Mazoezi ya kupiga danadana kabla ya mchezo wao...
Katibu wa Chama cha Waandoshi wa
Habari za Michezo Tanzania (Taswa) Amir Mhando akizungumza na wachezaji
wa Taswa kabla ya kuanza kwa michezo hiyo.
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja...
No comments:
Post a Comment