Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 30, 2011

Isha Mashauzi kumsindikiza Mkubwa Fella katika mpambano wa Nani mkali katika wasanii Kizazi kipya cha Taarab, tarehe 1 July. Equator Grill Temeke!.

Mkubwa FELLA
kiongozi wa kundi la bongo fleva TMK Family yakina Temba na Chegge, ambaye pia ni msanii chipukizi ktk Taarabu atachuana na wasanii wengine watatu chipukizi ktk miondoko hio ya muziki wa Taarabu ktk kumtafuta Mkali nani kati yao Ijumaa hii pale EQUATOR GRILL, Mtoni kwa Aziz Ally

Show hio ya aina yake itaanza mishale ya saa 2 usiku huku ikiongozwa na Kings Modern Taarab wanaotamba na nyimbo kibao kwasasa ikiwemo "Kijoka" na kusindikizwa na ISHA MASHAUZI mkali wa "Mama nipe Radhi" na zingine nyingi.

Wasanii wa kizazi kipya cha Taarab watakaopanda jukwaani kuoneshana nani mkali ni wale wanaotamba sana ktk medani hizo ambao ni Mkubwa Said Fella na nyimbo yake ya "Simuachi"aliyomshirikisha Isha, Athumani Ally "Nyongo mkalia ini", Omary Ally "Simuachi mpenzi wangu" na Kepteni Temba "Nimeiteka himaya".

Akimalizia kunihabarisha mratibu wa onyesho hilo la mpambano alisema kiingilio kitakuwa ni Tshs. 5000/= na wapenzi na mashabiki wote wa burudani kutoa maamuzi NANI MKALI KATI YAO!!!!!!

Tuesday, June 28, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MABALOZI WA KENYA, SUDAN NA ZAMBIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mavis Lengalenga, baada ya mazungumzo wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, John Mutinda Mutiso, wakati alipofika kumtembelea na kufanya mazungumzo ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo. Kushoto ni Msaidizi wa Balozi, Muthomi Muithiga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sudan Nchini Tanzania, Abdelbagi Hamdan Kabeir, wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo.

BURUDANI CLASSIC NDANI YA MZALENDO PUB JUMAPILI

BENDI mpya inayoundwa na wasanii wakali na chipukizi katika anga za muziki wa dansi, Mapacha wa3 wanatarajia kufanya onyesho la pamoja na wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanaotamba katika miondoko hiyo Julai 3 mwaka huu katika ukumbi wa Mzalendo Pub.
Wasanii hao ni pamoja na, Ali Kiba na Elias Barnaba maaarufu Barnabas, ambao watashambulia jukwaa moja na Mapacha wa3.
Mmoja wa wakurugenzi wa mapacha watatu Kharidi Chokoraa maarufu Tora bora amesema Onyesho hilo la pamoja litafanyika Jumapili Julai 3 katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama.
Chokoraa amesema lengo la onyesho hilo ni kuwapa ladha tofauti mashabiki wa Mapacha watatu na huenda ikafanyika kila Jumapili ya kwanza ya kila mwezi ili kudhihirisha kwa mashabiki ujio wao wa kutoa burudani hasa katika kiunga cha Mzalendo.
Aidha amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika nawasanii hao watapiga live na bendi hiyo, hivyo mashabiki watarajie kupata burudani ambayo hawajawahi kuipata kutoka kwa wasanii wa ndani.
“unajua Ali Kiba ni msanii mkubwa na ni mkali jukwaani na pia Barnaba ambaye amewahi kuimba na Faly Ipupa, alipokuja nchini na mapacha watatu ndo usiseme ni burudani ya kufa mtu.” Alisema Chokoraa.
Ali kiba amewahi kutamba na nyimbo kama Cinderela, mac Mugn, Karim na sasa anatamba na kibao cha Mapenzi yana run Dunia ambacho kimejizolea umaaarufu mkubwa wakati Barnaba ametamba na vibaon kama Njia panda na mbalamwezi, Nabembelezwa na sasa anaendelea kutamba na kutikisa na kibao chake cha Daima Milele.

SPIKA WA BUNGE APOKEA KOMBE

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwaonyesha waheshimiwa wabunge Kombe ambalo Ofisi ya Bunge imeshinda katika Maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha taasisi mbalimbali za Umma kutoka barani Africa na kufikia kilele wiki iliyopita tarehe 23 Juni, 2011. katika Maonyesho hayo Ofisi ya Bunge imekuwa mshindi wa Pili katika nafasi ya banda bora kwa utoaji bora wa huduma hususani katika kuelezea Kazi Bunge, Muundo wake, Mamlaka ya Bunge nk. picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
http://fullshangwe.blogspot.com/

Mkongo wa Taifa hauna madhara yoyote ya kiafya Waziri Charles Kitwanga

Na Lydia Churi-MAELEZO, DODOMA

Serikali imesema kupitisha mkongo wa taifa wa mawasiliano chini ya nyumba hakuna madhara yoyote kwa afya ya wananchi wanaoishi kwenye nyumba hizo wala kwa nyumba zenyewe.

Akijibu swali Bungeni mjini Dodoma leo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa Charles Kitwanga alisema Mkongo wa Taifa hauna madhara yoyote ya kiafya mahali unapopita kwa kuwa hupitishwa chini ya nyumba mita tatu kwenda chini.

Akifafanua, Mheshimiwa Kitwanga alisema wakati wa ujenzi wa mkongo huo, imebainika kuwa baadhi ya wananchi wamejenga nyumba ndani ya hifadhi ya barabara, hivyo ili kuendana na sheria ya hifadhi ya barabara, wizara imelazimika kupitisha mkongo chini ya nyumba hizo.

Aliongeza kuwa serikali inaangalia namna ya kulipa fidia kwa nyumba zilizobomoka baada ya kupitisha mkongo huo na fidia hiyo itatolewa kwa nyumba zilizokuwa zaidi ya mita 22 kama sheria ya zamani ya hifadhi ya barabara inavyosema. Kwa mujibu wa mabadiliko ya sheria ya hifadhi ya barabara, hifadhi ya barabara ni mita 30 kutoka katikati ya barabara.

Naibu waziri huyo alisema mkongo wa taifa wa mawasiliano hujengwa ndani ya hifadhi ya barabara, reli na nguzo za umeme za Tanesco ambapo wizara imekuwa ikiomba vibali kwa taasisi husika ili kutumia hifadhi hizo katika ujenzi wa mkongo huo.

Alisema sehemu kubwa ya mkongo wa taifa wa mawasiliano umewekwa kwenye hifadhi ya barabara zinazomilikiwa na TANROADS ambao wametoa kibali cha kujenga mkongo huo ndani ya mita moja ya mwisho ya hifadhi ya barabara yaani kati ya mita 29 na 30.

Mheshimiwa Kitwanga alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Kibiti Mheshimiwa Abdul Jabir Marombwa aliyetaka kujua ni kwa sababu gani mkongo wa taifa upitishwe chini ya nyumba za watu na ni madhara gani yanaweza kuwapata watu wanaoishi kwenye nyumba hizo.

Monday, June 27, 2011

NAPE AKUTANA NA WAMILIKI WA BLOGS, AZIPA BIG UP BLOG ZA BONGO

KATIBU wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, leo amekutana na wamiliki wa Blogs za Bongo na kubadilishana mawazo ikiwa ni sehemu ya kuboresha njia ya mawasiliano kupitia mtandao na hasa Blogs.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Nape alisema kuwa anazipongeza Blog zote kwa kuwa mstari wa mbele katia kuwafikishia ujumbe na habari kamili kwa wakati wananchi na kwamba amekuwa mstari wa mbele katika kufuatilia habari zinazotolewa kupitia blogs.
“Kwa upande wangu mimi ninakawaida ya kupitia Blogs zote kila asubuhi na jioni kabla ya kulala na kujionea mambo ambayo huenda siku ya pili naweza nisiyapate katika magazeti, kwa kweli nawapongeza sana kwa kazi zenu,
Na hili si kwa chama cha CCM pekee bali pia hata Serikali inatambua uwepo wenu na ndiyo maana mmekuwa mkitambulika kwa haraka zaidi na kufuatiliwa kila habari mnazozitoa katika blogs zenu” alisema Nape
Aidha nape aliwataka Mablogger kuendelea na jitihada za kuwahabarisha wananchi na kuwapa hata yale ya kuwarekebisha viongozi pale wanapoonekana kuzembea katika kazi zao.
Alitolea mfano wa Jengo la Sukita kuwa ni ndipo kilipoanzia Chuo Kikuu cha Dar es salaam, ambacho kwa sasa kimeshapiga hatua kubwa, lakini kuna watu bado hadi leo hii hawajui historia hiyo, hivyo kupitia Blogs wanaweza kufanya habari za uchunguzi na kuwaonyesha wananchi utofauti wa histotia kama hizo.
Nape pia aliwataka wanablogs hao kuwa naumoja wao yaani Chama cha Mablogger, jambo ambalo ajibiwa kuwa tayari ni watu wanaofanya kazi zao chini ya Ngao, na kuowaomba kutoa ushirikiano katika maandaliazi kuelekea sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, ili watu waweze kuona utofauti kati ya Enzi za Tano na CCM ya sasa.
“Lakini pia tumeanza maandalizi ya sherehe za kuzaliwa Chama cha Tano ambazo zitafanyika Julai 7 mwaka huu, kwa ajili ya kuwakumbusha wananchi chama chetu kilipoanzia” alisema Nape.
Aidha alisema kuwa CCM imeamua kukivunja Kitengo cha Propaganda na kuunga Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma ili kuweza kutoa na kupata taarifa kwa haraka na wakati.
Nape, akipozi kwa picha na baadhi ya wanablogger, baada ya kikao hicho. Kutoka (kushoto) ni Anthony Siame-Siamepix.Blogspot.com, Zainul Mzige-Mo Dewj Blog, Shamim Mwasha-8020 Fashion Blog, Mroki Mroki-Mrokim.blogspot,Nape Nnauye, katibu NEC, Muhidini Sufiani-Sufianimafoto.blogspot.com, ambaye ni mmiliki wa blog hii,Mtoto wa Kitaa.blogspot, Rajabu Mhamila Super D-Burudani mwanzomwisho.blog,Francis Dande, mwakilishi wa Michuzi Blog,Jofrey Mwakibete, mpigapicha wa Mo Dewj Blog, Othman Michuzi-Mtaa kwa Mtaa blog na Dj Choka-Dj Choka Blog.

Sunday, June 26, 2011

MWANAMUZIKI SHAGGY ATUA JIJINI MWANZA TAYARI KWA SERENGETI FIESTA CCM KIRUMBA KESHO

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Jaji Mark Bomani, akimkaribisha Mwanamuziki Shaggy kutoka nchini Marekani wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza, tayari kwa onyesho lake kabambe litakalofanyika katika tamasha la Msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Kesho.

Shaggy akipiga picha na warembo wawili mara baada ya kukabidhiwa ua kama ishara ya kumkaribisha wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza leo mchana.

Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo akisalimiana na mwanamuziki Shaggy mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza leo mchana.

Mtangazaji wa Clouds Rubeny Ncha kali akifanya mahojiano na mwanamuziki Shaggy mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

Mwanamuziki Shaggy akipozi kwa picha na warembo wa mwanza mara baada ya kwasili jijini huo leo mchana.

Mkurugenzi wa Clouds Entertainment Bw. Joseph Kusaga akimuongoza mwanamuziki Shaggy kutoka nchini Marekani mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza leo mchana.

http://fullshangwe.blogspot.com

BONDIA CHEKA AMDUNDA MKENYA KWA POINT

Bondia Francis Cheka akinyoshwa mkono juu na Refarii Omari Yazidu katikati wakati wa kutangaza mshindi picha na SUPER D BOXING COACH
Bondia Daniel Wanyonyi kushoto akitupa ngumi kwa bondia Cheka jana katika uwanja wa Jamuhuru Morogoro picha na Super D Boxing Coach

Bondia Wanyonyi akiendelea na Mashambulizi wakati wa mpambano uliofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro jana Cheka alishinda kwa point picha na Super D Boxing Coach
Asikali polisi wakimalisha ulinzi mkali uku wakiwa na mabomu ya kutoa machozi jana picha na Super D Boxing Coach

IRENE KALUGABA AWA VODACOM MISS MWANZA

Vodacom Miss Mwanza 2011 Irene Kalugaba akiwa a picha pamoja na =mshindi wa pili Vodacom Miss Mwanza Frola Razaro (kulia)a Monica James mshindi wa pili wa shindano la Vodacom Miss Mwanza lililofanyika kwenye hoteli mpya na ya kisasa kabisa ya Gold Crest karibu kabisa na hoteli kongwe ya New Mwanza Hoteli jijini Mwanza ambapo tayari shindano limekwisha na washindi ndioyo hao.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya ziwa Bw Stephen Kingu akipokea cheti kwa niaba ya Vodacom Tanzania kama ishara ya kampuni ya Sisi Entertainment kushukuru kwa udamini wao madhubuti na mnono kutoka Vodacom.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa Bw Stephen Kingu akiwa katika picha ya pamoja na wafayakazi wenzake, kulia ni Janet Kambeson msaidizi wa Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Miriam Makalla Mwakilishi wa Mauzo Vodacom Kanda ya Ziwa , Bernald Kombe Activation Coordinator Lake Zone .

Hii ndiyo tano bora ya Vodacom Miss Mwanza kutoka kulia ni Ester Laurent, Monica James, Diana James, Irene Kalrgaba na Frola Razalo wakipozi kwa picha.

Majaji wa shindano hilo wakijadili jambo kabla ya kumtangza mshindi kutoka kushoto ni Cess Odemba Ben Mwangi,Cynthia Buhama

Kutoka kulia ni Rubeny , Msanii Mwasiti , Zamaradi Mketema wakibembeleza mtoto.

Lina wa THT na Sajna msanii kutoka mkoani mwanza.

Msanii Barnaba akipagawisha mashabiki wake wakati wa shindano la Vodacom Miss Mwanza lililofanyika katika hoteli ya Gold Crest Hotel.

.Vazi la Ufukweni kama unavyoona.

Hapa wakiendelea kupita na vazi la ufukweni.

Vazi la Ufukweni bado linaendelea.

Wasanii wa mwanza wakifanya vitu vyao jukwaani wakati wa shindano la Vodacom Miss Mwanza linaloendelea usiku huu katika hoteli ya Gold Crest Hotel.

Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa Stephen Kingu katikati akiwa katika picha ya pamoja na wadau wengine wa Vodacom Mwanza wakishuhudia shindano hilo, Vodacom ni wadhamini wakuu wa Miss Tanzania

na Mkurugenzi wa Clouds Ruge Mutahaba

Mdau Flora kulia wa Mwanza akiwa na rafiki yake

Vazi la ubunifu

Hili limebuniwa kwa majani mapana yaliyokolea rangi ya kijani.

Hili limebuniwa kwa kitenge na shanga.

Mashabiki mbalimbali wa urembo wakishuhudia shindano hilo usiku huu.

Ukumbi umefurika kiasi kwamba hakuna mahali pa kukaa na watu wengine wameshindwa kuingia na kubaki nje na wengine kuondoka.

http://fullshangwe.blogspot.com/

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MADAWA YA KULEVYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Tatu Mapando, ambaye ni mmoja kati ya vijana waliotoa ushuhuda mbele ya Makamu wa Rais kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kuacha kutumia madawa hayo. Tatu aliwahi kuwa mnenguaji wa muziki wa dansi katika bendi za Fm, Academia, Diamond Sound, Betta Musica na bendi kadhaa za jijini kabla ya kuanza kutumia madawa.

Muelimisha Rika kutoka Banda la Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Catherine Saoke, akifafanulia jambo wanafunzi wa Shule ya Msingi, Kilimahewa ya Temeke, Mubaraka Abdallah na Ally Kionda, kuhusu utofauti na madhara kati ya dawa ya Cocaine na Heroin, wakati wanafunzi hao walipotembelea Banda hilo kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyokuwa katika moja ya mabanda hayo kwa ajili ya maonyesho.

Vijana waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya, Rajab Huseein na Tatu Mapando, wakitoa ushuhuda kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya baada ya kuacha kutumia madawa hayo.

MICHELLE OBAMA AKUTANA NA MANDELA AFRIKA KUSINI

First Lady Michelle Obama, left, with former South African President Nelson Mandela, at this home, in Houghton, South Africa. (Credit: Nelson Mandela Foundation,
First Lady Michelle Obama met with former South African President Nelson Mandela in Johannesburg on Tuesday in a private meeting at his home. Accompanied by daughters Sasha and Malia, as well as mother Marian Robinson,the first lady met with the iconic South African leader on the second day of a ten-day trip to Africa. The meeting marked the first time that Mandela, South Africa's first black president, and Mrs. Obama, America's first black first lady, had met. A photo shows Mandela, 92, sitting next to Mrs. Obama on the couch, signing a copy of his latest book for the first lady. The revered anti-Apartheid icon, who met Mr. Obama in 2006, was joined by his wife Graca Machel, the former first lady of South Africa and of Mozambique. Michelle Obama reportedly quipped to a greeter that her husband was "pouty" that he was unable to join the family on the trip, according to the Associated Press.

JB-ATWAA TUZO YA UIGIZAAJI BORA TAMASHA LA ZIFF ZANZIBAR

Msanii wa Luninga,JB (kushoto) akipokea Tuzo ya uigizaji Bora kutokaa kwa Ofisaa Mtendaji Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando
JB-akishangiliaa na kuifurahia Tuzo yake

Warembo wakiwa na tuzo mkononi tayari kwa kukaabidhiwaa kwa wahusika
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...