Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 26, 2011

IRENE KALUGABA AWA VODACOM MISS MWANZA




Vodacom Miss Mwanza 2011 Irene Kalugaba akiwa a picha pamoja na =mshindi wa pili Vodacom Miss Mwanza Frola Razaro (kulia)a Monica James mshindi wa pili wa shindano la Vodacom Miss Mwanza lililofanyika kwenye hoteli mpya na ya kisasa kabisa ya Gold Crest karibu kabisa na hoteli kongwe ya New Mwanza Hoteli jijini Mwanza ambapo tayari shindano limekwisha na washindi ndioyo hao.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya ziwa Bw Stephen Kingu akipokea cheti kwa niaba ya Vodacom Tanzania kama ishara ya kampuni ya Sisi Entertainment kushukuru kwa udamini wao madhubuti na mnono kutoka Vodacom.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa Bw Stephen Kingu akiwa katika picha ya pamoja na wafayakazi wenzake, kulia ni Janet Kambeson msaidizi wa Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Miriam Makalla Mwakilishi wa Mauzo Vodacom Kanda ya Ziwa , Bernald Kombe Activation Coordinator Lake Zone .

Hii ndiyo tano bora ya Vodacom Miss Mwanza kutoka kulia ni Ester Laurent, Monica James, Diana James, Irene Kalrgaba na Frola Razalo wakipozi kwa picha.

Majaji wa shindano hilo wakijadili jambo kabla ya kumtangza mshindi kutoka kushoto ni Cess Odemba Ben Mwangi,Cynthia Buhama

Kutoka kulia ni Rubeny , Msanii Mwasiti , Zamaradi Mketema wakibembeleza mtoto.

Lina wa THT na Sajna msanii kutoka mkoani mwanza.

Msanii Barnaba akipagawisha mashabiki wake wakati wa shindano la Vodacom Miss Mwanza lililofanyika katika hoteli ya Gold Crest Hotel.

.Vazi la Ufukweni kama unavyoona.

Hapa wakiendelea kupita na vazi la ufukweni.

Vazi la Ufukweni bado linaendelea.

Wasanii wa mwanza wakifanya vitu vyao jukwaani wakati wa shindano la Vodacom Miss Mwanza linaloendelea usiku huu katika hoteli ya Gold Crest Hotel.

Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa Stephen Kingu katikati akiwa katika picha ya pamoja na wadau wengine wa Vodacom Mwanza wakishuhudia shindano hilo, Vodacom ni wadhamini wakuu wa Miss Tanzania

na Mkurugenzi wa Clouds Ruge Mutahaba

Mdau Flora kulia wa Mwanza akiwa na rafiki yake

Vazi la ubunifu

Hili limebuniwa kwa majani mapana yaliyokolea rangi ya kijani.

Hili limebuniwa kwa kitenge na shanga.

Mashabiki mbalimbali wa urembo wakishuhudia shindano hilo usiku huu.

Ukumbi umefurika kiasi kwamba hakuna mahali pa kukaa na watu wengine wameshindwa kuingia na kubaki nje na wengine kuondoka.


http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...