Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 30, 2012

SAMSUNG YAZINDUA OFA YA MSIMU HUU WA SIKUKUU


 Meneja Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw. Syvester Manyara na Country Trainer wa Samsung Electronics Bw.Joel Laize wakionesha baazi ya simu zilizopo katika Ofa Maalumu ya msimu wa sikukuu ambapo watafanya Droo mbalimbali kwa washindi kujipatia zawadi kem kem kutoka kampuni hiyo 
SAMSUNG YAZINDUA OFA YA MSIMU HUU WA SIKUKUU
“Ni Draw ya zawadi kubwa kwa wateja watakaonunua bidhaa za Samsung”
KAMPUNI ya SAMSUNG Tanzania leo imezindua rasmi ofa maalum ya kipindi hiki cha sikukuu ijulikanayo kama “Samsung Season’s Offer!”. Uzinduzi huu umefanyika katika duka la Samsung lililoko Quality Centre, Dar Es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania Bwana Kishor Kumar alisema, “Ofa hii inalenga kuwazawadia wateja wetu zawadi hizi katika msimu huu wa sikukuu. Ofa hii imeanza rasmi leo Ijumaa tarehe 30 Nov na itaisha Jumamosi tarehe 5 Januari 2013.” Bwana Kishor alielezea zaidi kwamba wateja wote watakaonunua bidhaa za Samsung zilizo katika ofa hii watapata zawadi za papo kwa hapo na pia watapata nafasi ya kujishindia zawadi kubwa katika Draw ya mwisho. Draw ya mwisho itashuhudiwa na wasimamizi kutoka bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha na itafanyika katika duka la Samsung Quality Centre Jumapili tar 06 January mwakani.
Naye meneja usambazaji wa Samsung Mobile Tanzania Bwana Sylvester Manyara alisema kwamba, “Pamoja na bidhaa nyingine za Samsung, bidhaa zilizo katika ofa hii kabambe ni aina ya Galaxy Note 2, Samsung S3, Galaxy Note 10.1, Samsung S Duos, Samsung ACE Duos, Galaxy Pocket na Galaxy Pocket Duos.” Bwana Manyara aliendelea kuelezea kwamba wateja watakaonunua bidhaa za Samsung kipindi hiki watapata kuponi maalum ambazo watajaza na kuzikusanya ili kujaribu bahati yao katika Draw kubwa ya mwisho. Ofa hii inaendeshwa katika maduka ya Dar Es Salaam, na maduka ya Samsung yaliyoko Mbeya, Arusha, Dodoma na Mwanza.
Bwana Kishor Kumar alimaliza kwa kutaja zawadi zitakazotolewa kwamba ni;
1.    Zawadi ya Kwanza; Samsung LED TV ya Inchi 42’.
2.    Zawadi ya Pili; Samsung Galaxy S3 Mobile Phone.
3.    Zawadi ya Tatu; Samsung Galaxy Note 10.1.
4.    Zawadi ya Nne; Samsung Home theatre.
5.    Zawadi ya tano; Samsung Smart Camera.
Pamoja na zawadi hizi, Samsung itatoa zawadi kwa wateja mbalimbali watakaokutwa wakinunua bidhaa za Samsung, miongoni mwa zawadi hizi ni TV tatu za inchi 32 zitakazotolewa moja kila wiki kwa wiki tatu mfululizo kuanzia wiki hii.
Naye bwana Manyara alimaliza kwa kuwashukuru wateja wa Samsung kwa kuchagua bidhaa hizi bora, aliwaomba waendelee kufurahia bidhaa hizi hata baada ya kipindi cha msimu huu wa sikukuu. Aliwakumbusha kwamba miongoni mwa manufaa ya bidhaa za Samsung ni kwamba bidhaa zake ndio tu zina warantii ya miezi 24 yaani miaka miwili. Aliwakumbusha pia kupiga namba ya huduma kwa wateja endapo wakihitaji ufafanuzi kuhusu jambo lolote kuhusu bidhaa za Samsung. Namba ya huduma kwa wateja wa Samsung ni +255 685 88 99 00.
Samsung inaendesha kampeni hii ikiwa ni wiki chache baada ya kufanya maonyesho makubwa ya bidhaa zake jijini Dar Es Salaam yaliyofahamika kama “Samsung Week”. Samsung inafanya pia shughuli nyingi za kujitolea, hususani msaada wa udhamini wa mafunzo kuinua vipaji vya wanariadha katika shule ya Winning Spirit Arusha, msaada kwa shule na matibabu katika kijiji cha Ilmorijo Monduli Arusha na Lyamungu Moshi nk.

TAMADUNI MUZIKI KUZINDUA SANTURI NNE KWA PAMOJA


WASANII WAMLILIA SHARO MILIONEA KWA WIMBO MMOJA - KAZA MOYO


Video ya kumuenzi marehemu HUSSEIN a.k.a Sharo Milionea huu wimbo umeimbwa na Shetta, Dayna Nyange, shilole mohamed, Cannal Top, Rich Mavoko, Shadoo, Amazon, Barnabas Elias, Stamina, Dan rock, Suma Mnazaleti, Eric Mlindima, Muba c, Seif

BONGO ALL STARS together we canAudio producer ni C9Kanjenje 
Video directed by Msafiri under KWETU studio
R.I.P Sharo Milionea tutakukumbuka daima milele

TIBAIJUKA AZINDUA UJENZI WA NYUMBA 48 ZA NHC MCHIKICHINI DAR


 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa nyumba 48 za kuuza za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala Mchikichini, Dar es Salaam jana.Anayeongoza kupiga makofi kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu (kulia), akimkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Profesa Tibaijuka kuzindua mradi huo.
                        Waziri Tibaijuka akihutubiwa wakati wa hafla hiyo
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli  akihutubia
                                              Profesa Tibaijuka akikagua ujenzi huo
                                           Moja ya majengo yanayojengwa eneo hilo

CHADEMA YATATHMINI UHAI WA CHAMA KINONDONI



 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Willibrod Slaa akifungua Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kinondoni kuhusu Uhai wa Chama uliofanyika Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto ni Ofisa wa Sera na Utafiti wa Chadema, Mwita Mwikwabe Waitara na Naibu Katibu Mkuu Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Subira Waziri (wa tatu kulia). (Picha na Habari Mseto Blog)
 Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akizungumza na wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kinondoni
 Ofisa wa Sera na Utafiti wa Chadema, Mwita Mwikwabe Waitara
Baadhi ya wajumbe

Precision Air supports breast cancer screening in Mtwara and Lindi


Precision Air Commercial Director Mr. Patrick Ndekana (left) speaks to journalists (not in picture) in Dar es Salaam yesterday about his company’s support of 9m/- towards a four-days breast cancer awareness and screening campaign that kicks off in Mtwara and Lindi on Wednesday. Looking on is the Aga Khan Health Service’s Head of Nursing Services, Loveluck Mwasha. (Photo by our correspondent)
Aga Khan Health Service (AKHST’s) Head of Nursing Services, Loveluck Mwasha (right) speaks to journalists (not in picture) in Dar es Salaam yesterday about a four-days breast cancer awareness and screening campaign that kicks off in Mtwara and Lindi on Wednesday, which has received a support of 9m/- from Precision Air Services PLC. Looking on is the Precision Air Commercial Director Mr. Patrick Ndekana. (Photo by our correspondent)


By Correspondent 

Precision Air supports breast cancer screening in Mtwara and Lindi By Correspondent Precision Air (PW) has donated 9m/- geared towards supporting the breast cancer awareness and screening campaign that kicks off in Mtwara and Lindi on Wednesday.

 The four-day event that that will run under the theme “Check it, Beat it” is spearheaded by the Aga Khan Health Service, Tanzania (AKHST) and seeks to reach more women, especially those living in areas without sufficient access to health services. 

Speaking to reporters in Dar es Salaam yesterday, the Precision Air Commercial Director Patrick Ndekana said the donation is part of the Airline’s Corporate Social Responsibility Programme (CSR) that aims to promoting screening to reduce the need for major surgery or death cases faced by many Tanzanians. 

Ndekana said Precision Air understands the importance of heath in national development that is why it chose to support the campaign.

 “Our mission is to beat breast cancer by funding such projects that targets our remote communities who do not have access to proper health services nor the financial support to have major surgeries.

 We believe our support will go a long way in saving people’s lives because early detection saves lives.

 “Having our Airline presence in Mtwara, we are aware that the revenue we derive is from a healthy community. 

The airline will only do business if we have less number of people with ill-health. It is only a healthy people who form a healthy nation that brings forth a stable and ever growing economy. 

“Precision air will only continue growing in terms of increasing the number of its fleets and open more routes to serve more customers in this region. We can only achieve that when we have a strong and stable economy in countries we operate,” said Mr Ndekana. 

On her part, representative from Aga Khan Health Service, Tanzania (AKHST) Ms Loveluck Mwasha, Head of Nursing Services, mentioned that the campaign which will be carried in Mtwara and Lindi Regions is targeting a population of 4 million people while at least 500 women are expected to be screened between the two towns.

 The campaign is targeting women, young and old in these two towns - for the Breast Cancer Screening - but will also see men being screened for the same. Ms Mwasha said that an initial site visit to Mtwara and Lindi was made by the Breast Cancer Campaign Team, including the AKHST Medical Director, Dr. Jaffer Dharsee, and Mr. Sisawo Konteh, Head of Outreach Services, of the Aga Khan Health Service, Tanzania, during which they met with the Regional Medical teams in both towns and agreed on the camp models.

 Every year, thousands of Tanzanian women are diagnosed with breast cancer. It is a major life altering event for women who are diagnosed, but for some the diagnosis comes much too late. 

Globally, breast cancer is among the leading causes of cancer-related deaths in women. Early detection of the disease through breast cancer awareness and screening campaigns is vital to reducing the devastating prevalence of this disease amongst women in East Africa.

 Today, Precision Air calls for all citizens in Mtwara to “Check it, Beat it!”

DESIGNERS LINE UP FOR TANZANIA RED RIBBON FASHION GALA 2012


Organiser of Tanzania Red ribbon Fashion Gala Ms.Khadija Mwanamboka (second from right) at the group photo with some of the designers at her Office.
Founder and Chairperson of Tanzania Mitindo House (TMH) Ms. Khadija Mwanamboka together with the Kids from the Tanzania Mitindo House Orphanage Centre.

“My Dream is to be a top designer” One of the Orphan get trained for free at Tanzania Mitindo House Office.
***********************
DESIGNERS AND MODELS – FIRST ROUND
MOROGORO POLYTEX - VITENGE
1. EVE COLLECTIONS
a)Ava
2. SALIM ALI
a) Ben
3. MARTIN KADINDA
a) Alexia
4. EDNA SILVER
a) Nadia
5. GABRIEL MOLLEL
a) Hidaya
6. SHELLINA IBRAHIM
a) Neema
7. FRANKOO DESIGNS
a) Elgiver
8. Hameed
a) Victor
9. ASIA IDARIOUS KHAMSIN
a) Jamila
TANZANIA RED RIBBON FASHION GALA 2012
FASHION SHOW – SECOND ROUND
DESIGNERS AND MODELS
1. MUSTAFA HASSANALI
a) Jamila
b) Elgiver
c) Alexia
2. Hameed Abdul
a) Ben
b) Hidaya
3.SHELLINA IBRAHIM
a) Neema
b) Jamila
4.GABRIEL MOLLEL
a) Nadya
b) Ava
5.EDNA SILVER
a) Neema
b) Ben
7.EVE COLLECTIONS
a)Ava
b) Hidaya
6. SALIM ALLY
a)Neema
b)Victor
8. MARTIN KADINDA
a) Nadia
b) Alexia
9.FRANKO DESIGNS
a)Ben
b)Victor
10.ASIA IDARIOUS KHAMSIN
a) Elgiver
b)Jamila

AIRTEL Tanzania kumpongeza Balozi wake AY katika Bonge la Party ndani ya Nyumbani Lounge


Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde na Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) kwa pamoja wakionyesha tuzo ya  Channel 'O'  aliyoipata Mwanamuzi huyo nchini Afrika Kusini. Tukio hilo limefanyika leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY kwa ushindi alioupa pamoja na kumwandalia sherehe ya kumpongeza itakayofanyika leo usiku nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY balozi wake kwa kupata tuzo ya chanel O ya video bora, Katikati ni AY  akifatiwa na DJ wake Athur Baraka.

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava)  na Balozi wa Ambwene Yessaya 'AY' akiwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kumwezesha kupata tuzo hiyo kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na kushoto ni  DJ wake Athur Baraka.
****************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na balozi wake Ambwene Yessaya “AY” leo wamewashukuru watanzania kwa kumpigia kura msaani maarufu wa kizazi kipya Ambwene Yessaya  “ AY “  na kumwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most Gifted East African video of the Year kupitia kibao chake kipya kijulikanacho kama “   I don’t wanna be alone”

Akiongea na wandishi wa habari katika Ofisi za Airtel leo AY amechukua fulsa kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kuweza kumwezesha kuibuka na ushindi. Aidha alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea kushirikiana naye katika kufikisha habari na kumsaidia kupata tuzo hiyo.

Naye Afisa uhusino wa Airtel Jane Matinde alisema” tunafurahi kuona msanii AY ambaye ni balozi wetu kuibuka na tuzo iliyoshirikisha wasanii mbalimbali toka  Afrika, sisi tunasikia furaha kuona mafanikio ya wasanii wetu nchini yakiendelea kukua na ndio sababu leo tuko hapa kusherehekea ushindi  huu kwa pamoja na kuwashukuru watanzania kwa kumuwezesha AY kupata tuzo hii kwa kura zenu.

Tunapenda pia kuchukua fulsa hii kuwaalika watanzani na wateja wetu leo pale nyumbani lounge usiku kuanzi saa tatu tuweze kujumuika na AY na kumpongeza kupata tuzo hii. Tutakuwa na wasanii wengi pamoja na wadau mbalimbali wa Musiki na pia utapata muda kupiga picha na msanii huyo na Tuzo yake

ZANZIBAR HEROES ILIVYOICHAPA RWANDA NA NIYONZIMA 'NDANI' JANA 2-1


Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakisujudu wakati wakishangilia goli lao la kwanza lililofungwa wakati wa mechi yao ya Kundi C la Kombe la Chalenji kwenye Uwanja wa Mandela, Kampala leo.
Selemani Kassim 'Selembe' wa Zanzibar Heroes akiwatoka wachezaji wa timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi) wakati wa mechi yao ya Kundi C la michuano CECAFA Challenge kwenye Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Namboole nchini Uganda jana. Zanzibar Heroes walishinda 2-1. Habari na Picha kwa hisani ya Straika Blog
**********************
LICHA ya mazingira magumu ya uwanja uliojaa tope kama shamba la mpunga, timu ya Zanzibar Heroes walipambana kishujaa na kushinda kwa magoli 2-1 mechi yao ya Kundi C la Kombe la Chalenji jijini Kampala dhidi ya Rwanda jana jioni. 


Nyota wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, Khamis Mcha 'Viali' alifunga mara mbili na kuifanya Zanzibar ifikishe pointi 4 baada ya mechi mbili na sasa ina uhakika wa kutinga hatua ya 8-Bora hata kwa nafasi ya ‘best looser’ kulingana na matokeo ya mechi za mwisho. 

Rwanda inayoshika nafasi ya pili ya msimamo wa Kundi C kwa kuwa pointi 3 na Malawi iliyo katika nafasi ya tatu kwa pointi 3 pia baada ya jana kushinda 3-2 dhidi ya Eritrea inayoburuza mkia, zinaweza kufikisha pointi 6 zikishinda mechi zao za mwisho Jumamosi. Hata hivyo, matokeo hayo hayataizuia Z’bar kutinga robo fainali kama ‘best looser’, endapo itapoteza mechi yake ya mwisho Jumamosi dhidi ya Malawi. 

Hali mbaya ya uwanja iliwagharimu pia Malawi na Eritrea, ambapo katika matukio mawili -- moja kwa kila timu -- mpira uliokuwa ikiserereka kuingia wavuni ulikwama kwenye dimbwi la maji kabla ya kuokolewa na mabeki wa timu hizo. 

Katika tukio la kwanza wakati Malawi wakiongoza kwa magoli 2-0 wangeweza kufunga goli la tatu baada ya mpira kumpita kipa na mchezaji mchezaji wa malawi kupiga shuti dogo katika lango tupu akidhani amefunga lakini mpira ulikwama kwenye dimbwi kabla ya beki kufika na kuokoa mpira.

Tukio jingine lilikuja wakati Eritrea wakiwa nyuma kwa magoli 2-1 na wangeweza kufanya matokeo yawe 2-2 lakini mpira uliokuwa ukienda wavuni ulinasa kwenye dimbwi na kuwapa nafasi Malawi kuokoa.  

Zanzibar ilipata goli la kuongoza katika dakika ya 9, shukrani kwa madimbwi ya maji yaliyouzuia mpira usimfikie kipa wa Rwanda, Jean Claude Ndoli, aliyekuwa katika nafasi nzuri ya kuuokoa jirani na ukingo wa boksi na kumpa mwanya Mcha kufunga katika nyavu tupu.

Mcha alifunga goli la pili katika dakika ya 62 kufuatia pasi ndefu kutoka kulia.

Rwanda walicharuka na kupata goli kupitia kwa Dady Birori aliyefunga kwa kichwa katika dakika ya 80 kufuatia krosi ‘matata’ ya nahodha Haruna Niyonzima.

Kocha wa Rwanda, Milutin Sredjovich ‘Micho’ alisema baada ya mechi hiyo kwamba hawezi kusingizia uwanja kwa kipigo chao kwa sababu hata wapinzani wao walicheza katika uwanja huo huo lakini alisema mazingira yalikuwa hayafai kuendelea kuchezewa mechi.

Michuano hiyo inaendelea kesho kwa mechi za Kundi A ambapo Kenya itacheza dhidi ya Ethiopia saa 10:00 jioni kabla ya wenyeji Uganda ambao tayari wametinga robo fainali watawakaribisha Sudani Kusini saa12:00 jioni.

MKUTANO MKUU WA NAMANGA SPORTS CLUB KUFANYIKA DESEMBA 09 NDEGE BEACH


Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, David Mwaka akiongoza kikao cha maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa Klabu, kilichofanyika Leecar's Pub Namanga jijini Dar es Salaam. PICHA/JOHN BADI
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

- KONYAGI yaupiga 'Jeki'

Na John Badi
 
Mkutano Mkuu Maalum wa Klabu ya Namanga Sports unatarajiwa kufanyika Desemba 09, mwaka huu katika Ukumbi wa Ndege Beach uliopo katika eneo la Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi, Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, Bw. David Mwaka alisema tayari makampuni kadhaa yameshajitokeza kudhamini mkutano huo.

Bw. Mwaka aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Tanzania Distilleries Ltd watengenezaji wa kinywaji maarufu cha Konyagi, Mike Commercial, Esoshi General Trading Co. Ltd na Mele DJ Co. Ltd ya Dodoma.

"Tunawashukuru sana wadhamini ambao tayari wamekwisha onyesha moyo wa kutusaidia, lakini pia tunawaomba wadhamini wengine wajitokeze zaidi ili tuweze kufanikisha mkutano wetu", alisema Bw. Mwaka.

Aidha Bw. Mwaka alitoa wito kwa wanachama wa klabu hiyo ambao bado hawajatoa michango yao ya 20,000/- kuiwasilisha mara moja kwa watu waliopewa majukumu ya kukusanya ambao ni John Gako, Bebee Mangi na Chale JJ.

BOB CHORA AMNG'ARISHA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE'


Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake unaokuja zidi ya bondia Saidi Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake wa DESEMBA 9
MOJA YA BANGO LILILOCHOLWA NA BOB CHORA
Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake unaokuja zidi ya bondia Saidi Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake unaokuja zidi ya bondia Saidi Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Thursday, November 29, 2012

TIGO NA REACH FOR CHANGE YAKABIDHI DOLA ZA KIMAREKANI 75,000 KWA WASHINDI WATATU KILA MOJA KUPITIA SHINDANO LA WAJASIRIAMALI KUTPITIA SHINDANO LA REACH FOR CHANGE


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Andrew Hodgson (Kushoto) akiwa na mmoja wa wajasiliamali aliyeshinda shindano la Tigo Reach For Change, Bi. Brenda D. Shuma pamoja na Mkurugenzi wa Reach For Change Sarah Damber.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Andrew Hodgson (Kushoto) akiwa na washindi watatu wa shindano la Tigo Reach For Change,  Bi. Brenda D. Shuma, Nyabange Chirimi na Thadei Msumanje, kulia ni Mkurugenzi wa Reach For Change Bi.  Sarah Damber.
 Mmoja wa wajasiliamali aliyeshinda shindano la Tigo Reach For Change, Bi. Brenda D. Shuma akielezea jambo kwa waandishi wa Habari.
Meneja wa Tigo, kitengo cha huduma za Jamii Woinde Sishael akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari na wadau walihudhuria mkutano huo.
Wadau wakifuatilia kwa umakini.
---
Mwezi Septemba mwaka huu, Tigo kwa kushirikiana na Shirika la kujitolea la Reach For Change kwa mara ya kwanza nchini Tanzania walizindua programu iliyodhamiria kutambua na kuendeleza mawazo madhubuti ya wajasiriamali  yenye lengo la kuboresha maisha ya watoto.
Baada ya kampeni ya mwezi mmoja ya kutoa wito kwa watanzania wote wenye mawazo madhubuti kujitokeza kwa ajili ya ajili ya kuwasilisha maombi yao, tulipokea maombi 2480, ambapo waombaji 15 walifika fainali  ikifuatiwa na mchujo mkali ambao ulijumuisha wafanyakazi wa Tigo na Reach For Change pamoja na wataalamu wengine wa nje. Hawa waliendelea kuchujwa hadi tulipofanikiwa kupata washindi watatu  baada ya mawazo yao kupitishwa na jopo la majaji.
"Mpango wa kurejesha kwa Jamii sehemu ya faida yetu, ni moja ya nguzo ya kampuni yetu na tuna nia ya dhati na mpango huu wa Reach for Change, ambao ni sehemu ya mpango wetu kimataifa. Tigo Tanzania imepokea maombi yenye mvuto na ushindani wa hali ya juu. Washindi wa nafasi tatu za juu ambao wamechaguliwa leo si tu walishinda mioyo za majaji bali waliwavutia na ubunifu wa mipango yao dhubuti. Sasa waanapokea ufadhili wa $25,000 kama mshahara wa mwaka, kwa miaka mitatu mfululizo ili kuweza kuzingatia na kutimiza malengo yao," alisema Andrew Hodgson, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tigo.
Washindi wa shindano la wajasiriamali la Tigo Reach For change mwaka 2012 ni Brenda-Deborah Shuma, Nyabange Chirimi na Thadei Msumanje. Miradi yao watakayo ianzisha italenga katika kuwawezesha watoto wenye ulemavu na vijana wenye ujuzi wa kiufundi, kusaidia elimu ya watoto wa mitaani na kuboresha elimu kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).
'Tigo Reach for Change' imelenga katika kuainisha na kusaidia wajasiriamali kwenye miradi ya kijamii na wenye mawazo yakinifu juu ya kuboresha maisha ya watoto wa Tanzania. Washindi hawa watatu sasa wanajiunga na programu ya miaka mitatu ya kuboresha miradi yao, ambapo mawazo yao yatabadilishwa kuwa miradi endelevu. Mbali na hayo, watapata mshahara wa dola 25,000 kwa mwaka kwa miaka mitatu mfululizo pamoja na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wafanyakazi waandamizi wa Tigo.
Reach for Change ni Shirika la kujitolea lililoanzia Sweden ambalo lilianzishwa na Kinnevik, ambaye ndiye aliyeunda kampuni ya Millicom (shirika anzilishi la Tigo). Kampeni ya kutafuta wajasiriamali kwa mkakati wa Reach for Change kwa mara ya kwanza ulianzia huko Sweden mwaka 2010 ikifuatiwa na Russia 2011 kabla mwaka huo huo kuanzishwa barani AfriKa katika nchi ya Ghana. Hadi sasa imeweza kuboresha maisha ya watoto wapatao 140,000 nchini Ghana.
Tigo na Reach For Change imeanza rasmi utafutaji wa wajasiriamali kwenye miradi ya kijamii,  katika nchi zinazotoa huduma yake barani  Afrika, kwa kuzinduliwa kwanza Rwanda ikifuatiwa na Tanzania, halafu Ghana, Congo DRC, Senegal na mwishomi itakuwa Chad miezi michache ijayo.

SBL YAZINDUA BIA YA TUSKER LITE DAR



Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon (wapili kulia) , akiwa pamoja na wafanyakazi wa SBL wakigonganisha chupa zao za Tusker Lite kuashiria furaha ya kuzinduliwa kwa  bia hiyo mpy. Tusker Lite ilizinduliwa wakati wa tafrija maalum ya ‘Markerts Night’ jijini Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wakiwa na mmoja wa washindi wa shindano maalum la uchezaji mziki lililofanyika katika usiku maalum wa Maafisa masoko jijini Dar es Salaam jana. Mshindi huyo wa pili alizawadiwa Glass maalum ya Tusker Lite, bia mpya iliyozinduliwa usiku huo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Epraim Mafuru (mwenye suti kushoto) akimkabidhi zawadi ya Tusker Lite, Meneja bidhaa wa Push Mobile, Gonzoga Rugambwa  baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa shindano maalum la uchezaji mziki lililofabnyika wakati wa uzinduzi wa bia ya Tusker Lite sanjari na usiku wa maafisa masoko jijini Dar es Salaam jana
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakifuatilia matukio mbalimbali wakati bia mpya ya Tusker Lite ilipozinduliwa sanjari na usiku maalum wa maafisa masoko jijini Dar es Salaam jana.B

BENDI YA MASHUJAA NA JB MPIANA KUZINDUA 'RISASI KIDOLE' KESHO IJUMAA


 Wanamuziki wa bendi ya Mashujaa, wakiongozwa na Chalz Baba (katikati) wakijifua wakati wa mazoezi yao ya maandalizi ya uzinduzi wa Albam yao ya pili inayokwenda kwa jina la Risasi Kidole, uzinduzi unaotarajia kufanyika kesho katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, huku ukisindikizwa na mwanamuziki mahiri kutoka Congo, JB Mpiana.
Kiongozi wa bendi hiyo, Chalz Baba, akiongoza mashambulizi wakati wa mazoezi hayo ya maandalizi leo.
************************
BENDI ya Mashujaa kesho siku ya Ijumaa itazindua albamu yake ya pili ijulikanayo kwa jina la Risasi Kidole pamoja na bendi maarufu ya Congo, Wenge BCBG iliyochini ya mwanamuziki JB Mpiana kwenye  viwanja vya Leaders club, Kinondoni.
Uzinduzi huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa meneja wa bendi ya Mashujaa, Martin Sospeter. Sospeter alisema kuwa wamejiandaa vilivyo katika uzinduzi huo na lengo lao kubwa ni kuweka historia katika muziki wa Tanzania.
Alisema kuwa wamekaa kambini muda wa siki mbili na wameandaa vitu vingi vipya kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki wa dansi nchini. Alisema kuwa kuna rap ya Ua Mbu na Dume la Simba kutoka kwa marapa wao, Saulo Ferguson na Sauti Radi.
Alifafanua kuwa wanamuziki wake wameadhimia ‘kufunika’ katika uzinduzi huo kwani anahistoria nzuri katika muziki wa Tanzania na kufanya kazi katika bendi nyingi.
“Tunawaomba watanzania waje waone nini tunakifanya mbele ya gwiji la muziki wa dansi Afrika, JB Mpiana, najua wao wamepania, lakini sisi tumepania vilivyo kusafisha nyoyo za mashabiki ambazo kwa sku nyingi hawajapata burudisha la mioyo zao,” alisema.
Kiongozi wa bendi hiyo, Charlz Baba alisema kuwa wamepania kutoa somo kwa wanamuziki wa dansi hapa nchini ambao wamekuwa wakisubiri waone watafanya nini. Alisema kuwa wameandaa nyimbo nyingi nzuri  na wamepatia kutawala soko la muziki hapa nchini.
“Njooni muone nini tunafanya katika muziki wa dansi, kambi yetu imekuwa nzuri na mafanikio makubwa, naomba mashabiki waje kutuunga mkono nasi tutawaunga mkono kwa kutoa burudani safi,”alisema Chalz.
Albamu ya Risasi Kidole ina jumla ya nyimbo sita. Nyimbo hizo ni Umeninyima, Tikisika, Hukumu ya Mnafiki, Ungenieleza, Kwa Mkweo na wimbo uliobebab jina la albamu hiyo, Risasi Kidole

WAANDISHI WA HABARI WAPATIWA MAFUNZO YA JUU YA SHERIA YA HAKI YA KUPATA HABARI.


Waandishi wa habari na wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka maeneo mbalimbali wakishiriki mafunzo kuhusiana sheria ya haki ya kupata habari pamoja na sheria ya huduma ya vyombo vya habari ili kuchangia uwepo wa vipengele vipya katika katiba mpya ambayo mchakatowake unaendelea.
Waandishi wa habari na wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka maeneo mbalimbali wakishiriki mafunzo kuhusiana sheria ya haki ya kupata habari pamoja na sheria ya huduma ya vyombo vya habari ili kuchangia uwepo wa vipengele vipya katika katiba mpya ambayo mchakatowake unaendelea.

Baadhi ya wanasemina hao wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI CHARLES TIZEBA ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE.


Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akipata malezo kutoka kwa Afisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), Bw. Elieza Mwalutende, wakati Naibu Waziri huyo alipotemmbelea Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl . Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanja hicho.

Hayo ni Majenereta yanayotumika endapo Umeme wa TANESCO unapokatika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijjini Dar es Salaam.

UNGANA NA SKYLIGHT BAND WEEKEND HII


SOKO LA BUGURUNI RELINI YAENDELEA KUKUA KWA KASI


Hili ni moja ya soko linaloshamili kwa kazi sana jiji Dar es Salaam (lipo Buguruni relini) japo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifumbia macho si salama kwa afya za binadamu na usalama kwa ujumla. Napenda kusema kuwa watendaji wetu wameshindwa kukomesha na kuliondoa kabisa mambo mbali mbali yanayoendelea kinyume cha sheria. ANGALIZO: Mamlaka muhimu ni vyema ikachukua sheria muhimu kuzuia hali hii inayotokea ili kuepusha majanga yanayotokea mbeleni.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...