Baadhi
ya Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa wanasubiri treni ya mwakyembe iwasili
stesheni ikitokea ubungo maziwa tayari kwa safari ya kuwarudisha
Majumbani Kwao.
Abiria
wakianza kupanda treni tayari kwa kurejea makwao mara baada ya treni la
mwakyembe kuwasili kituoni hapo kwenye majira ya saa kumi na moja na
dakika ishirini jana.
Mmoja
wa Abiria aliyegeuza na treni hilo aliyepandia Kituo cha Kamata, kwa
lengo la kuwahi kiti akibishana na mmoja wa abiria aliyechini katika
foleni.
Wakazi
wa Jiji la Dar wakiwa kwenye foleni ya kupanda treni maarufu kwa jina
la treni ya mwakyembe jana kwenye majira ya saa 11 jioni katika kituo
cha Stesheni.
Wakazi
wa jiji la Dar wakipanda kwenye treni la mwakyembe mara baada ya
kuwasili kwenye kituo chake cha Stesheni jana Kwenye majira ya Saa 11
Jioni, tayari kwa kuwarudisha majumbani kwao likitokea Mjini kuelekea
Ubungo ambapo ndio kituo cha Mwisho.
**************************
**************************
ABIRIA
wanaotumia usafiri wa Treni, nao wameiga staili ya abiria wa Mbagala,
ambapo hulazimika kila jioni na asubuhi abiria katika kituo cha Treni
cha Stesheni kupanda Treni hilo na kugeuza nalo, jambo ambalo huwafanya
abiria wanaosubiria usafiri huo mwisho wa kituo kukosa nafasi na siti
kutoka na treni hilo kufika kituoni likiwa tayari limejaa.
Abiria
waliokuwa wakisubiria treni hilo walianza kulalamika baada ya kuona
kila behewa likiwa tayari limeshajaa kabla hata treni hiyo haijafika
kwenye kituo chake cha mwisho kwa lengo la abiria hao kuwahi .
Baada ya Tukio hilo kutokea kulizuka sintofahamu kwa baadhi ya wafanyakazi na Askari Polisi ambao hawajawahi kuona utaratibu huo ukifanyika na kupelekea Abiria kuhisi tayari wafanyakazi wa treni hiyo waneshaanza kuchakachua kitu ambacho utaratibu hauruhusu.
Baada ya Tukio hilo kutokea kulizuka sintofahamu kwa baadhi ya wafanyakazi na Askari Polisi ambao hawajawahi kuona utaratibu huo ukifanyika na kupelekea Abiria kuhisi tayari wafanyakazi wa treni hiyo waneshaanza kuchakachua kitu ambacho utaratibu hauruhusu.
No comments:
Post a Comment