Tigo na Reach For Change yakabidhi $75,000 kwa
washindi watatu kila mmoja kutekeleza miradi yao kupitia Shindano la
wajasiriamali la Reach for ChangeDar es Salaam, Tanzania, 28 Novemba, 2012. Mwezi Septemba mwaka huu, Tigo kwa
kushirikiana na Shirika la kujitolea la Reach For Change kwa mara ya kwanza
nchini Tanzania walizindua programu iliyodhamiria kutambua na kuendeleza mawazo
madhubuti ya wajasiriamali yenye lengo la
kuboresha maisha ya watoto. Baada ya kampeni ya mwezi mmoja ya kutoa wito kwa
watanzania wote wenye mawazo madhubuti kujitokeza kwa ajili ya ajili ya
kuwasilisha maombi yao, tulipokea maombi 2480, ambapo waombaji 15 walifika
fainali ikifuatiwa na mchujo mkali ambao
ulijumuisha wafanyakazi wa Tigo na Reach For Change pamoja na wataalamu wengine
wa nje. Hawa waliendelea kuchujwa hadi tulipofanikiwa kupata washindi watatu baada ya mawazo yao kupitishwa na jopo la
majaji.
"Mpango wa kurejesha kwa Jamii sehemu ya faida
yetu, ni moja ya nguzo ya kampuni yetu na tuna nia ya dhati na mpango huu wa
Reach for Change, ambao ni sehemu ya mpango wetu kimataifa. Tigo Tanzania imepokea
maombi yenye mvuto na ushindani wa hali ya juu. Washindi wa nafasi tatu za juu
ambao wamechaguliwa leo si tu walishinda mioyo za majaji bali waliwavutia na
ubunifu wa mipango yao dhubuti. Sasa waanapokea ufadhili wa $25,000 kama
mshahara wa mwaka, kwa miaka mitatu mfululizo ili kuweza kuzingatia na kutimiza
malengo yao," alisema Andrew Hodgson, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tigo.
Washindi wa shindano la wajasiriamali la Tigo Reach
For change mwaka 2012 ni Brenda-Deborah Shuma, Nyabange
Chirimi na Thadei Msumanje. Miradi yao watakayo
ianzisha italenga katika kuwawezesha watoto wenye ulemavu na vijana wenye ujuzi
wa kiufundi, kusaidia elimu ya watoto wa mitaani na kuboresha elimu kupitia
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).
'Tigo Reach for Change' imelenga katika kuainisha na
kusaidia wajasiriamali kwenye miradi ya kijamii na wenye mawazo yakinifu juu ya
kuboresha maisha ya watoto wa Tanzania. Washindi hawa watatu sasa wanajiunga na
programu ya miaka mitatu ya kuboresha miradi yao, ambapo mawazo yao
yatabadilishwa kuwa miradi endelevu. Mbali na hayo, watapata mshahara wa dola
25,000 kwa mwaka kwa miaka mitatu mfululizo pamoja na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wafanyakazi
waandamizi wa Tigo.
Reach for Change ni Shirika la
kujitolea lililoanzia Sweden ambalo lilianzishwa na Kinnevik, ambaye ndiye
aliyeunda kampuni ya Millicom (shirika anzilishi la Tigo). Kampeni ya kutafuta
wajasiriamali kwa mkakati wa Reach for Change kwa mara ya kwanza ulianzia huko
Sweden mwaka 2010 ikifuatiwa na Russia 2011 kabla mwaka huo huo kuanzishwa
barani AfriKa katika nchi ya Ghana. Hadi sasa imeweza kuboresha maisha ya
watoto wapatao 140,000 nchini Ghana.
Tigo na Reach For Change imeanza
rasmi utafutaji wa wajasiriamali kwenye miradi ya kijamii, katika nchi zinazotoa huduma yake barani Afrika, kwa kuzinduliwa kwanza Rwanda
ikifuatiwa na Tanzania, halafu Ghana, Congo DRC, Senegal na mwishomi itakuwa Chad
miezi michache ijayo.
No comments:
Post a Comment