Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo,
Andrew Hodgson (Kushoto) akiwa na mmoja wa wajasiliamali aliyeshinda
shindano la Tigo Reach For Change, Bi. Brenda D. Shuma pamoja na
Mkurugenzi wa Reach For Change Sarah Damber.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo,
Andrew Hodgson (Kushoto) akiwa na washindi watatu wa shindano la Tigo
Reach For Change, Bi. Brenda D. Shuma, Nyabange Chirimi na Thadei
Msumanje, kulia ni Mkurugenzi wa Reach For Change Bi. Sarah Damber.
Mmoja wa wajasiliamali aliyeshinda
shindano la Tigo Reach For Change, Bi. Brenda D. Shuma akielezea jambo
kwa waandishi wa Habari.
Meneja wa Tigo, kitengo cha huduma za
Jamii Woinde Sishael akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari na
wadau walihudhuria mkutano huo.
---
Mwezi
Septemba mwaka huu, Tigo kwa kushirikiana na Shirika la kujitolea la
Reach For Change kwa mara ya kwanza nchini Tanzania walizindua programu
iliyodhamiria kutambua na kuendeleza mawazo madhubuti ya
wajasiriamali yenye lengo la kuboresha maisha ya watoto.
Baada ya kampeni ya mwezi mmoja ya
kutoa wito kwa watanzania wote wenye mawazo madhubuti kujitokeza kwa
ajili ya ajili ya kuwasilisha maombi yao, tulipokea maombi 2480, ambapo
waombaji 15 walifika fainali ikifuatiwa na mchujo mkali ambao
ulijumuisha wafanyakazi wa Tigo na Reach For Change pamoja na wataalamu
wengine wa nje. Hawa waliendelea kuchujwa hadi tulipofanikiwa kupata
washindi watatu baada ya mawazo yao kupitishwa na jopo la majaji.
"Mpango wa kurejesha kwa Jamii sehemu
ya faida yetu, ni moja ya nguzo ya kampuni yetu na tuna nia ya dhati
na mpango huu wa Reach for Change, ambao ni sehemu ya mpango wetu
kimataifa. Tigo Tanzania imepokea maombi yenye mvuto na ushindani wa
hali ya juu. Washindi wa nafasi tatu za juu ambao wamechaguliwa leo si
tu walishinda mioyo za majaji bali waliwavutia na ubunifu wa mipango
yao dhubuti. Sasa waanapokea ufadhili wa $25,000 kama mshahara wa
mwaka, kwa miaka mitatu mfululizo ili kuweza kuzingatia na kutimiza
malengo yao," alisema Andrew Hodgson, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tigo.
Washindi wa shindano la wajasiriamali
la Tigo Reach For change mwaka 2012 ni Brenda-Deborah Shuma, Nyabange
Chirimi na Thadei Msumanje. Miradi yao watakayo ianzisha italenga
katika kuwawezesha watoto wenye ulemavu na vijana wenye ujuzi wa
kiufundi, kusaidia elimu ya watoto wa mitaani na kuboresha elimu
kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).
'Tigo Reach for Change' imelenga katika kuainisha na kusaidia wajasiriamali kwenye miradi ya kijamii
na wenye mawazo yakinifu juu ya kuboresha maisha ya watoto wa
Tanzania. Washindi hawa watatu sasa wanajiunga na programu ya miaka
mitatu ya kuboresha miradi yao, ambapo mawazo yao yatabadilishwa kuwa
miradi endelevu. Mbali na hayo, watapata mshahara wa dola 25,000 kwa
mwaka kwa miaka mitatu mfululizo pamoja na ushauri wa kitaalamu kutoka
kwa wafanyakazi waandamizi wa Tigo.
Reach for Change ni Shirika la
kujitolea lililoanzia Sweden ambalo lilianzishwa na Kinnevik, ambaye
ndiye aliyeunda kampuni ya Millicom (shirika anzilishi la Tigo).
Kampeni ya kutafuta wajasiriamali kwa mkakati wa Reach for Change kwa
mara ya kwanza ulianzia huko Sweden mwaka 2010 ikifuatiwa na Russia
2011 kabla mwaka huo huo kuanzishwa barani AfriKa katika nchi ya Ghana.
Hadi sasa imeweza kuboresha maisha ya watoto wapatao 140,000 nchini
Ghana.
Tigo
na Reach For Change imeanza rasmi utafutaji wa wajasiriamali kwenye
miradi ya kijamii, katika nchi zinazotoa huduma yake barani Afrika,
kwa kuzinduliwa kwanza Rwanda ikifuatiwa na Tanzania, halafu Ghana,
Congo DRC, Senegal na mwishomi itakuwa Chad miezi michache ijayo.
No comments:
Post a Comment