Na Elizabeth John
MUIGIZAJI wa filamu nchini, Mohamed Nurdin
‘Chekibudi’ ameonekana kupanda katika soko la filamu baada ya kuachia filamu
yake inayokwenda kwa jina la ‘Dikteta’, ambayo imeanza kufanya vizuri sokoni.
Filamu hyo mpya inayoonesha
ukandamizaji wa familia, imekamilika na kuingizwa sokoni hivi karibuni, ambapo
tayari imeanza kufanya vizuri katika
mauzo, katika baadhi ya maeneo ya jijini
Dar es Salaam, ikisambazwa na kampuni ya steps Entertaiment.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Chekibudi amesema, filamu hiyo ameiandaa ili kuonesha ukandamizaji
uliopo baadhi ya familia katika maisha ya kila siku, na amefarijika kuona iko
katika wakati mzuri sokoni.
Alisema baada ya kuangalia
hilo, aliamua kuweka wazo lake katika filamu ili kuwafikishia ujumbe watu wengi
zaidi na ikawa kama ni moja ya kazi za wasanii kuelimisha na kufundisha jamii.
“Unajua unapokuwa msanii
unatakiwa kuwa mbunifu katika mambo mengi na ndiyo maana kila kukicha
tunaangalia ni jinsi gani tutawakumbusha wenzetu matatizo ambayo yanaepukika,”
amesema Chekibudi.
Chekibudi alishawahi kufanya
vizuri alipokuwa katika kundi la sanaa la ‘Splendid’, na katika filamu hiyo ya
‘Dikteta’ amewashirikisha nyota wengine kama, Cojack, Philipo, Munira Sultan,
Snura Mush, Coletha Reymond pamoja na nyota wengine.
No comments:
Post a Comment