Kikosi cha Harambee Stars katika picha ya pamoja
Mshambuliaji Victor Wanyama akiwa na mlinda mlango wa Harambee Stars
Arnold Origi, ambao wanasadikika kuwa hawatocheza pambano dhidi ya Taifa
Stars, licha ya kutua nchini leo na timu yao.
Na Irene Mark
Nao wachezaji wa Yanga waliokuwa na klabu yao jijini
Tanga kwa ajili ya pambano lao dhidi ya Coastal Union, wamewasili jijini humo jana
mchana, tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa kesho saa 10:00 alasiri
KIKOSI cha wachezaji 23 na viongozi 10 wa timu ya Taifa ya Kenya
‘Harambee Stars,’ kimetua jijini Mwanza leo saa 2:30 asubuhi, kwa ajili ya pambano la
kimataifa la kirafiki, dhidi ya wenyeji Taifa Stars litakalofanyika kesho
Jumatano kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Habari zilizoifikia Habari Mseto kutoka jijini humo zinapasha kuwa,
Harambee
Stars imewasili kwa ndege ya Precision na kushukia kwenye uwanja wa
ndege wa
Mwanza tayari kwa mtanange huo, huku ikidaiwa kuwa nyota wake wawili
hawatocheza pambano hilo, licha ya kutua nchini na kikosi chao.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, nyota wa Celtic ya Uskochi, Victor Wanyama
aliyefunga bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2-1 wa Celtic dhidi ya
FC Barcelona ya Hispania, ni miongoni mwa nyota wa kulipwa walioambatana
na kikosi hicho, ingawa inadawa hatocheza sambamba na kipa Arnold
Otieno.
chanzo chetu kiewataja wachezaji waliotua na kikosi hicho
kuwa ni Arnold Otieno, Dennis Oliech, Victor Wanyama, Ayub Masika, Brian
Onyango, Patrick Oboya na Patrick Osiako, Jerry Santo na Fredrick Onyango.
Wengine waliomo kwenye kikosi hicho ni Edwin Wafula, Eugene Asike,
Geofrey Odhiambo, Mulinge Ndeto, Christopher Nyangweso, James Situma, Peter
Opiyo, Charles Okwemba, Francis Wambura, Andrew Tololwa, Osborne Monday, Wesley
Kemboi na Moses Arita.
Viongozi watakaoambatana na kikosi hicho ni pamoja na Kocha
Henry Michel, anayesaidiwa na Mohammed Boujarari, huku viongozi wengine wakiwa
ni Florent Louis Robert Motta, Sunil Shah, Wycliff Makanga, Wilberforce Juma,
Benson Otieno, Ali Rehan, Robert Akumu na Angeline Nzavi.
Aidha, Osiah aliongeza kuwa, wachezaji wa Yanga waliokuwa na
klabu yao jijini Tanga kwa ajili ya pambano lao dhidi ya Coastal Union, Frank
Domayo, Simon Msuva na Athuman Chuji na Kelvin Yondani, wamewasili jijini Mwanza
jana mchana, tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa kesho saa 10:00 alasiri.
Osiah alimaliza kwa kutaja viingilio vya mechi hiyo, ambapo
alisema vitakuwa ni shilingi 15,000 kwa watazamaji wa Jukwaa Kuu, huku wale wa
mzunguko wakitakiwa kulipa shilingi 5,000 kuliona pambano hilo lililo kwenye
kalenda ya Fifa.
No comments:
Post a Comment