Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda,
wakati wa hafla ya uzinduzi wa uwanja huo iliyofanyika mkoa Mpya wa
Katavi, leo katika uwanja huo baada ya kukamilika kwa ukarabati
uliogharimu kiasi cha Sh. Bilioni 30. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, (kushoto) ni Mama Zakhia Bilal (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu
wa Miundombinu, Omar Chombo na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt.Charles
Tizeba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifunua kitambaa kuweka jiwe la msingi, kuashiria uzinduzi rasmi wa
Uwanja wa Ndege wa Mpanda, uliopo Mkoani Katavi. Uzinduzi huo umefanyika
leo katika uwanja huo uliopo Mkoa wa Katavi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na Mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kikundi cha
sanaa cha Hiyari ya Moyo chenye maskani yake, Mpanda mjini, wakati
walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mpanda, leo kwa ajili ya kuzindua
rasmi uwanja huo na Mkoa wa Katavi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na Mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kikundi cha
sanaa cha Mama Monica, chenye maskani yake, Maji Moto Mpanda mjini,
wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mpanda, leo kwa ajili ya
kuzindua rasmi uwanja huo na Mkoa wa Katavi.
Mbunge
mstaafu, Chrisant Mzindakaya, akijumuika na wasanii wa ngoza ya asili
kucheza ngoma ya kabila la Wakonongo wa Inyonga, wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, uliofanyika sambamba na uzinduzi
wa mkoa mpya wa Katavi.
No comments:
Post a Comment