LONDON, England
Wakati akitambia kile alichofanya mwaka huu, Murray ‘Muzza,’ hakusita
kusifu kiwango cha mpinzani wake Roger Federer, ambaye alimng’oa katika fainali
za ATP kwa seti mbili za 7-6 6-2 na kutinga fainali alikoumana jana na Novak
Djokovic.
NYOTA wa tenisi duniani, Andy
Murray (pichani juu/kulia), amejipongeza kwa mng’aro aliopata mwaka huu, katika tasnia ya mchezo
huo.
Tambo za kinara huyo wa tenisi
Uingereza, zimekuja wakati akishindwa kuwika katika fainali za dunia za ATP
World Tour, akitambia mafanikio yake katika mashindano ya Olimpiki na ubingwa
wa michuano ya wazi ya Marekani ‘US Open.’
Wakati akitambia alichofanya mwaka huu, Murray ‘Muzza,’ hakusita kusifu kiwango cha mpinzani
wake Roger Federer, ambaye alimng’oa katika fainali za ATP kwa seti mbili za
7-6 6-2 na kutinga fainali alikoumana jana na Novak Djokovic.
Murray akafunguka akisema:
“Federer alicheza vema. Mimi nilianza vizuri, kisha naye akaja vema na kushinda
mchezo.
“Ni vigumu sana kumzuia wakati
anapokuwa amekutangulia na kimsingi nilimpa faida kubwa na ikawa ngumu kwangu
kurejea uongozi.
“Ningefurahishwa kama
ningefanikiwa kumakliza mwaka huu kwa kutwaa ubingwa wa fainali hizi tukuka.
“Lakini kwangu mimi ulikuwa ni
mwaka bora kulinganisha na mingine katika kipindi kilichopita cha uchezaji tenisi
kilicho na umbali mrefu. Naangalia nyuma kwa mtazamo chanya, nikiamini
sikukosea pakubwa sana.”
No comments:
Post a Comment