Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 16, 2012

THE AFRICAN TOUR -BILL MUSIC CONCERT


 Maryse Ngalula  Mwanamuziki kutoka DRC
Elie Kamano ‘ General Kamano’ Kulia ambaye ni kutoka nchini Guinea.
Dar es Salaam ,Tanzania
Akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani  ambapo alifichua siri na kusema kuwa yeye anatoka katika familia ya Machifu  nchini humo lakini amekimbia kuwa Chifu   na kukimbilia muziki ambao anasema unampatia kipato  ipasavyo licha ya kwamba alilazimika kufukuzwa nyumbani na babake mzazi.
 
"Babangu hakupenda niwe mwanamuziki ili nije niwe kiongozi kwetu  lakini kwa kuwa kuwa napenda sana muziki nimejikuta nikiziacha mila na kuendelea na muziki  hadi sasa"anasema

Taasisi  ya Kituo cha Utamaduni Cha Ufaransa kesho jioni wameandaa onesho la bure muziki wa utamaduni wa mwafrika.
Akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari Ofisa Habari wa kituo hicho Michael Shuma aliwataja wasanii watakaonogesha kuwa ni Maryse Ngalula  anayetoka Kinshansa Jahuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.
Elie Kamano ‘ General Kamano’ anayetoka nchini Guinea anayepiga muziki wake katika miondoko ya Hip Hop.
Katika tamasha hilo wasanii hao wawili watatumbuiza mmojammoja na baadaye watatoa burudani kwa kuimba pamoja.
Wakati huohuo  Koshuma aliongeza kwamba  Kituo cha Utamaduni Cha Ufaransa kimekuwa na utaratibu wa kufanya maonesho la utamaduni.

“Sisi tupo kwa ajili ya kutangaza Utamaduni wa Mtanzania hivyo nyote mnakaribishwa”.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...