LIONEL MESSI AVUNJA REKODI YA MABAO YA PELE
BARCELONA, Hispania
Mabao 76 aliyofunga, ni tisa
nyuma ya Gerd Muller anayeshikilia rekodi ya kudumu, wakati Pele alikuwa
akishika nafasi ya pili – akiwa ametikisa nyavu mara 75 akiwa na klabu yake ya Santos na timu ya taifa ya Brazil mwaka 1958
MWANASOKA Bora wa Dunia kwa
miaka mitatu mfululizo, Lionel Messi, juzi amethibitisha kuwa ni bora kuliko
nyota wa zamani wa soka duniani Edson Arantes do Nescimento ‘Pele’ na hilo ni
rasmi kwa sasa na halina mjadala.
Messi nyota wa klabu ya FC Barcelona
na timu ya taifa ya Argentine, ameivunja rasmi rekodi ya mabao ya Pele shujaa
wa Brazil
– aliyofunga kwa upande wa klabu na timu ya taifa katika kalenda ya mwaka.
Mkali huyo aliye katika
kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya nne mfululizo ya Balon d’Or, alifunga mara
mbili katika ushindi wa Barca wa mabao 4-2 dhidi ya Mallorca
na kumfanya afikishe idadi ya mabao 76 kwa mwaka huu wa 2012.
Idadi hiyo, ni mabao tisa nyuma
ya Gerd Muller anayeshikilia rekodi ya kudumu, wakati Pele alikuwa akishika
nafasi ya pili – akiwa ametikisa nyavu mara 75 akiwa na klabu yake ya Santos na timu ya taifa ya Brazil mwaka 1958.
Kocha wa Barca, Tito Vilanova hakusita
kuizungumzia rekodi hiyo, akisema: “Rekodi ya Leo ni ya kuvutia mno.
“Ni ya kuvutia zaidi wakati
unapofikiria juu ya ukweli kwamba, amefunga mabao mengi zaidi kwa mwaka, ambao
kimsingi haujaisha.
"Baadhi ya wachezaji ufunga
idadi hiyo ya mabao katika kipindi cha misimu kati ya saba hadi nane, yeye
amethubutu kufanya hivyo katika mwaka mmoja. Na mengi kati ya hayo ni mabao ya
ufundi zaidi.”
Messi mwenye rekodi ya kusisimua
dimbani katika misimu saba mfululizo ya ligi, anaongoza mbio za Kiatu cha
Dhahabu msimu huu akiwa na mabao yake 15, huku akiwa ametikisa nyavu mara 20
katika mashindano yote ya msimu huu.
No comments:
Post a Comment