Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 23, 2012

VIONGOZI WALIOIBA MAMILIONI KATORO WAFUNGWE-CCM




* Asema kuwapa uongozi Chadema ni sawa na kumkabidhi Bucha Fisi
NA BASHIR NKOROMO, GEITA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Katoro Mazemule  na wenzake wanaodaiwa kuhusika na wizi wa sh. milioni 16.5 za Halmashauri ya kijiji hicho wafikishwe mahakamani haraka.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo, katika mji mdogo wa Katoro, mkoani Geita, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema, ni lazima wahusika wote wa wizi wa fedha hizo wafikishwe mahakamani kwa kuwa ni jasho la wananchi.

Fedha hizo zinadaiwa kuliwa na Mwenyekiti huyo kwa tiketi ya Chadema, katika kipindi cha mwaka 2010 na 2011 hali ambayo imezusha tafrani miongoni mwa wananchi na uongozi wa Halmashauri ya Kijiji hicho hadi sasa.

Nape alisema, ni lazima Mwenyekiti huyo na waliohusika wote wafikishwe mahakamani kwa kuwa kamati iliyoundwa kuchunguza upotevu wa fedha hizo ilishamaliza kazi yake na ripoti kukabidhiwa kwa mamlaka zinazohusika.

"Kamati ya kuchunguza wizi wa fedha hizi ambazo ni mali ya wananchi ilishafanya kazi yake na kukabidhi ripoti kwa mamlaka zinazohusika, sasa kinachosubiriwa ni nini wahusika hawa kupelekwa mahakamani?", Nape alihoji na kuongeza;

"Sasa CCM kwa kuwa ndicho chama tawala, tunaagiza hatua za kuwapeleka mahakamani wahusika wote zichukuliwe haraka ili haki itendeke".

Nape alisema, kutotokea kwa wizi wa fedha hizo chini ya uongozi wa Halmashauri ya Kijiji hicho ambao upo chini ya chama hicho, ni dalili kwamba kujidai kwao kuwa wasafi na wapigania haki za wanyonge ni sawa na kilio cha mamba.

" Kila mara tumekuwa tukiwaambia acheni kuhadaiwa na Chadema, hawa siyo chama cha siasa ni kundi la wajanja fulani, sasa Wana Katoro mmejionea wenyewe, mmewajaribu mkawapa halmashauri yenu, fedha wamezitafuna sasa mnahangaika", alisema na kuongeza;

"Kwa kuwa mmepata funzo hili, bila shaka hamtaruidia tena, kwani mmeshafahamu kwamba kuikabidhi uongozi Chadema ni sawa na kumkabidhi fisi bucha".

Mapema, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma, alisema kwenye mkutano huo kwamba, kama hatua za kuwafikisha mahakamani wahusika hazitachukuliwa haraka, ataongoza wananchi wa Katoro kuandamana ili kuhakikisha hatua hizo zinachukuliwa.

Kabla ya mkutano huo, NMape alifungua shina la wajasiriamali la CCM, Bugayambele lenye wanachama  53 ambao hushughulika na kazi za kutengeza fenicha mbalimbali katika karakana yao iliyopo eneo hilo la Katoro.

Akifungua shina hilo, Nape aliahidi kuwapa sh. milioni moja kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao, ikiwa ni pamoja na kununua vitendea kazi kama randa za mbao, mashine ya kuchetrza mbao na ujenzi wa banda kwa ajili ya shughuli hizo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...