Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 22, 2012

Benki ya Azania yachangia milioni tano kusaidia kampeni dhidi ya saratani ya tezi dume



 Mkurugenzi wa Benki ya Azania, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (Usimamizi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara) Bw. Godwin Seiya (kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mratibu wa kampeni dhidi ya Saratani ya tezi dume inayojulikana kama  ‘Tanzania 50 Plus Campaign’ Dk.Emmanuel Kandusi (katikati) ikiwa ni msaada wa benki hiyo katika Kampeni hiyo. Kulia ni Mratibu kutoka Shirika lisilo la kiserikali la SAHRiNGON Martina Kabisama. Na Mpiga Picha Wetu.
 Mkurugenzi wa Benki ya Azania, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (Usimamizi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara) Bw. Godwin Seiya (katikati) akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mratibu wa kampeni dhidi ya Saratani ya tezi dume inayojulikana kama ‘Tanzania 50 Plus Campaign’ . Kushoto ni Mratibu wa kampeni hiyo Dk.Emmanuel Kandusi na kulia ni Mratibu kutoka Shirika lisilo la kiserikali la SAHRiNGON Martina Kabisama.
Mratibu wa kampeni dhidi ya Saratani ya tezi dume inayojulikana kama ‘ Tanzania 50 Plus Campaign’ Dk.Emmanuel Kandusi (kushoto) akisisitiza jambo kwa wanaandishi wa habari kabla ya kupokea hundi ya shilingi milioni tano kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya Azania katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (Usimamizi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara) Bw. Godwin Seiya (katikati) ikiwa ni  msaada wa benki yake katika Kampeni hiyo.


Na Mwandishi Wetu

BENKI ya Azania imechangia shilingi milioni tano kuiunga mkono kampeni ya Tanzania 50 Plus inayolenga kujenga uelewa kwa wananchi dhidi ugonjwa wa saratani ya tezi dume (Prostate Cancer).

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Benki ya Azania, ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (Usimamizi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara) Bw. Godwin Seiya alisema benki yake itaaendelea kusaidia programu mbalimbali za kijamii ndani ya jamii inayoizunguka benki hiyo.

Alisema benki yake ipo katika mchakato wa kuandaa sera maalum itakayo simamia shughuli mbalimbali za benki zinazolenga kuisaidia jamii na kusisitizia kuwa sera hiyo itaeleza kikamilifu mchango wa benki yake kwenye suala la kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii huku akisema kuwa uamuzi huo utafikiwa baada ya makubaliano na wanahisa wa benki hiyo.

Alibainisha kuwa benki yake imeamua kusaidia kampeni hiyo ya Saratani ya tezi dume iliikusaidia kuhamasisha wananchi kufanya vipimo angalau mara moja kwa mwaka, na kuongeza kuwa kupitia jitihada hizo itsaidia kupunguza hatari ya kuwa na waathirika wengi wa ugonjwa huo sbaadae.

"Takwimu zinasema ni watu 1000 wanaofariki kwa ugonjwa wa saratani kila mwaka Tanzania.Saratani ya tezi dume imaua mwanaume moka kila dakika 13. Sisi kama Benki ya Azania tunaamini kuwa njia pekee ya kupunguza hathari ya ugonjwa huu ni kupitia kampeni ya kujenga uelewa katika jamii.

"Kwa minajili hiyo basi sisi kama Benki ya Azania tunaona namna moja ya kudhibiti ni kwa uenezi wa taarifa zake kwa watu wachukue tahadhari paaale inapowezekana kuepukana na ugonjwa huu," aliongeza.
Kwa upande wake Mratibu wa kampeni hiyo ya Tanzania 50 Plus Dk.Emmanuel Kandusi ambae pia ni muhanga wa saratani ya tezi dume wakati wa tukio hilo alisema maisha ya watu wengi yataokolewa kama watu wataamua kufanya uchunguzi wa hiari katika umri mdogo kati ya miaka 45 na 50.

"Ugonjwa huu ni hatari. Mara nyingi watu wengi huamua kwenda hospitali pale ugonjwa unapofikia hatua mbaya. Ni muhimu kwa wnaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea kuweka kipaumbele tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya tezi dume angalau mara moja kwa mwak, "aliongeza.

Aidha, Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la SAHRiNGON Martina Kabisama alitoa wito kwa makampuni mengine na watu binafsi kuiunga mkono kampeni hiyo ili kampeni hiyo ilete matokeo yaliyo chanya kwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...