Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro akionesha zawadi ya taa ya kutumia mionzi ya jua
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah akibonyeza kitufe cha kompyuta kuwatafuta washindi wa promosheni hiyo.
Meneja
wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah (wa pili kulia)
akiangalia namna washindi wa promosheni ya Ki-College Zaidi na NMB
wanavyopatikana wakati wa droo ya kwanza iliyochezeshwa Makao Makuu ya
benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkaguzi wa Michezo ya
Kubahatisha, Humudi Abdulhussein. Kushoto ni Meneja wa Amana, Boma
Raballa na Meneja Masoko, Shilla Senkoro
Na Salum Mkandemba
BENKI ya NMB, leo imewazawadia wanafunzi wawili wa Chuo
Kikuu Dodoma (UDOM), Chacha Nyange Nchamcho na Kelvin Gabone, kila mmoja zawadi
ya I Pad, katika promosheni ya Ki-COLLEGE Zaidi inayoendeshwa na benki hiyo.
Promosheni hiyo inayohusisha wanafunzi wenye akaunti ya NMB
Student, ilifanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo
washindi wengine wawili walijishindia simu za mkononi aina ya Samsung Galaxy.
Jumla ya washindi 66 walipatikana katika droo hiyo, ambapo
60 kati yao walijishindia zawadi za taa maalum za kujisomea zinazotumia mionzi
ya jua, fulana za NMB, jezi za Taifa Stars na ongezeko mara mbili la kaunti ‘Amana
Maradufu.’
Akizungumza wakati wa promosheni ya kuwasaka na hatimaye
kuwatangaza washindi hao, Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro, aliwataka
wanafunzi kuendelea kufungua akaunti ya NMB Student au kuweka amana zao, ili
kujishindia zawadi mbalimbali katika droo mbili zijazo.
Droo hiyo iliyochezeshwa chini ya Ofisa Mkaguzi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha nchini, Humud Abdulhussein, ni ya Oktoba, ambapo
washindi wa mwezi huu watasakwa mwezi ujao, huku wateja wa droo ya mwisho ya
Desemba, watatafutwa Januari mwakani
Senkoro aliongeza kuwa, nia ya promosheni hiyo ni kurudisha
sehemu ya faida yao kwa wateja, hususani wanafunzi kupitia akaunti maalum
iliyoanzishwa mwaka 2007, kutokana na ongezeko la vyuo vya elimu ya juu nchini
vilivyoongeza idadi ya wateja.
Alisema kuwa, hadi sasa akaunti ya NMB Student ina zaidi ya
wanafunzi 70,000, waliofungua katika matawi mbalimbali nchini, huku akiwataka
wengine kuendelea kujitokeza ili kujishindia zawadi zitakazotoa msukumo wa
maendeleo yao kimasomo.
No comments:
Post a Comment