Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia
waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa
Babati wakati wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa hilo Usharika wa
Babati,Mkoani Manyara leo.
Mbunge wa
Jimbo la Babati Vijijini,Mhe. Jitu Vrajlal Soni (wa tatu kulia)
akizungumza wakati wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani Manyara
leo.Wengine pichani toka Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye
Harambee hiyo),Mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri na Kulia ni
Diwani wa kata ya Endamilay (CCM) Gesso Bajuta.
Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimpongeza
Mbunge wa Viti maalum Mkoani Manyara (Chadema),Mh. Pauline Gekul mara
baada ya kuchangia kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani Manyara leo.Kulia
ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini,Mhe. Jitu Vrajlal Soni.
Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiendelea
kupokea michango mbali mbali kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani Manyara
leo.
Baadhi ya
Waumini wa Kanisa hilo wakiwa kwenye Harambee hiyo ya Ujenzi wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa
Babati,Mkoani Manyara leo.
Na mwandishi wetu
Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh Edward Lowassa amesema wakati
umefika sasa hapa nchini elimu ya sekondari iwe ni elimu inayotolewa
bure na kumwondolea mwananchi mzigo .
Lowassa
amesema hayo leo mjini Babati wakati wa harambee ya ujenzi wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati.
Alisema kwa
sasa kila kata hapa nchini ina shule ya sekondari na huo ulikuwa mpango
wake akiwa Waziri Mkuu na alisimamia kikamilifu suala hilo na kufanikiwa
kwa asilimia mia moja.Shule hizo za kata ni maarufu kama shule za
Lowassa.
Hata hivyo kiwango kinachotolewa na shule hizo ni cha chini sana.
Waziri Mkuu
huyo mstaafu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli alisema sasa
wakati umefika kwa kila mtanzania kulizungumzia suala hilo bila ya woga
hususani wadau wa elimu na kuongeza kuwa.
''Ni lazima
tukubali na tujadili suala hilo kwa manufaa ya nchi kwa kila mtanzania
kukubali ushauri huo wa elimu ya sekondari kuwa ya bure''alisisitiza na
kuongeza kuwa kuwa ni vyema baada ya kulijadili suala hilo la elimu ya
bure ya sekondari tena elimu iliyo bora liwemo kwenye ajenda za Chama
cha Mapinduzi (CCM) za uchaguzi mkuu wa 2015.
Lowassa
alisema kuwa hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alitoa wito kwa shule za
sekondari kujenga maabara kwa wingi,hivyo kwa hiyo amesema ni suala
linalopaswa kuungwa mkono na kila mtanzania na pia elimu ya bure katika
sekondari nayo inapswa kuungwa mkono.
‘’Nasema sasa
wakati umefika elimu ya sekondari kuwa kama elimu ya msingi kwa watoto
kusoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ‘’alisema.
Lowassa
aliwaasa pia wadau mbalimbali hapa nchini kuwa mstari wa mbele kuchangia
elimu ili nchi hapo baadae iwe na vijana wenye elimu ya kutosha na ya
hali ya juu.
No comments:
Post a Comment