Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Waziri wa Elimu na Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, (wa pili kulia)
wakikata utepe kwa pamoja kuashiria kuzindua jengo jipya la Ofisi za
Veta mkoa wa Mtwara na Lindi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa
Uimarishaji wa ajira kupitia mafunzo ya Ufundi Stadi katika Chuo cha
Ufundi cha VETA mkoani Mtwara. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo Nov
26, 2012 Mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Simba
Kalia (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa VETA nchini, Eng.
Zebadia Moshi na (kulia) ni Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam, Idrisa
Msholo.
Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa VETA nchini, Eng.
Zebadia Moshi, wakati alipokuwa kitembelea kukagua jengo jipya la VETA
lililopo Mkoani Mtwara, baada ya kulizindua rasmi leo Nov 26, 2012. Wa
pili (kushoto) ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa ajira
kupitia mafunzo ya Ufundi Stadi, Chuo cha Ufundi VETA mkoa wa Mtwara,
leo Nov 26, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Moham med Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Chuo cha VETA, Lupakisa
Mapamba, kuhusu matumizi wa mashine ya kuchana mbao, wakati
alipokuwa akitembelea katika Karakana za Chuo hicho wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa ajira kupitia Mafunzo ya Ufundi
Stadi ya Chuo cha VETA, uliofanyika leo Nov 26, 2012 Mkoani Mtwara. Wa
nne (kushoto) ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal.
No comments:
Post a Comment