Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 15, 2012

MAMIA WAMZIKA MARIAM KHAMIS


MAREHEMU MARIAM KHAMIS
VILIO, majonzi na simanzi leo alasiri vimetawala katika mazishi ya mwimbaji mahiri wa taarabu nchini wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT), Mariam Hamis 'Paka Mapepe' (26) aliyefariki jana alfajiri Jijini  Dar es Salaam kutokana na matatizo ya uzazi.
Mariam ambaye amewahi kuimba bendi mbalimbali za taarabu nchini alifariki Dunia juzi usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akizungumzia kifo cha masanii huyo shangazi wa marehemu ambaye alimlea, Chiku Abdalah alisema marehemu alifikishwa hospitali ya Sinza kwa ajili ya kujifungua, lakini hali yake ilionekana kuwa mbaya zaidi hivyo kupelekwa hospitali ya Mwananyamala na baadaye Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Chiku alifafanua zaidi kwamba kifo cha Mariam ambacho kilitokana na kifafa cha uzazi, ambapo alipofanyiwa oparesheni hakufanikiwa kuamka mpaka kifo chake.
Shangazi huyo alisema awali marehemu hakuwahi kuugua magonjwa ya kifafa, hivyo familia inaamini ni matokeo ya kawaida katika uzazi na kuendelea kuamini kifo chake ni mipango ya Mungu.
Kwa upande wa wasanii waliowahi kufanya kazi na Mariam akiwemo Leyla Rashidi mke wa Mzee Yusuph alisema msanii huyo, atakumbukwa katika tasinia ya taarabu kutokana na mchango mkubwa alioutoa akiwa na umri mdogo.
"Kwa kweli huu msiba ni mkubwa katika muziki wa taarabu, tena tumeumia mno ndiyo mana tunashindwa kuvumilia lakini yote ni mipango ya Mungu, Mariam atakumbukwa kwa mchango wake na pia wasanii tutajitolea kuhakikisha tunaienzi familia yake, kwa kila tulichonacho baada ya msiba," alisema.
BLOG HII IKIWA NI MDAU WA MUZIKI WA TAARAB INATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU , WASANII NA WADAU  WOTE WA MUZIKI HUOU PIA NAUNGANA NA KILA ALIYEGUSWA NA MSIBA HUU KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE.INNALILLAHWAINNA ILAIH RAJIUN

1 comment:

  1. It is really so easy and user helpful that even a newbie can use it.

    This clearly suggests that link speeds are inadequate with this protocol.


    Have a look at my blog post; obd2 scan tool

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...