Balozi wa Safari Lager Wezesha, Janeth Karabu(kushoto)
akiwaelimisha wakazi wa Iringa Mjini kuhusu Safari Lager Wezeshwa awamu ya pili
Mkoani hapo mwishoni mwa wiki.
Balozi wa Saafari Lager Wezesha, Sarafina Msawe(katikati)
akiwaelimisha wakazi wa Iringamjini kuhusu programu ya Safari Lager
Wezeshwa awamu ya pili iliyozinduliwa
mwinshoni mwa wiki Mkoani hapo.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL)
kupitia bia yake ya Safari Lager leo
inatarajia kuzindua rasmi msimu wa pili wa programu ya kuwaelimisha
wajasiriamali wa jijini Mbeya juu ya “Safari
Lager Wezeshwa”.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar Es Salaam jana Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
alisema timu ya Mabalozi 15 wa ya kuelimija jamii imeshawasili jijini Mbeya
tayari kuanza kutoa elimu kwa jamii ya wakazi wa Mbeya hasa wafanyabiashara
ndogo ndogo na wa kati juu ya programu ya Safari Wezeshwa.
Alisema Shelukindo, timu hiyo
ilianzia Mkoani Kilimanjaro,Arusha,Mwanza,Shinyanga,Morogoro,Iringa na Tanga
ikielimisha jamii ya Watanzania juu ya programu hiyo na sasa leo ni jijini Mbeya
ambapo watafanyakazi katika viwanja vya Malimbali vya jijini Mbeya kwa siku mbili
wakielimisha jamii juu ya Safari Lager Wezesha
na baada ya hapo watahamia Mkoani Lindi na Mtwara.
Programu hii ilipata mafanikio makubwa, mwaka jana
iliwawezesha wajasiriamali 54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya
biashara na ruzuku za vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi
milioni mia mbili. Bwana Shelukindo alisema, “Safari Lager kwa mara ya
pili inawaletea wamiliki wa biashara
nafasi ya kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii
inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa
ruzuku nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika
harakati za kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaoingia
na kufuzu vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia hasa ya Safari
Lager ni kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia
mafanikio katika kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii
inayowazunguka”.Alifafanua kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo
wadogo na sio wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya
programu hiini kutoa hamasa kwa wajasiriamali
kote Tanzania ili wajitahidi zaidi
katika shughuli wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze
kufikia ndoto zao. Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama
fedha taslimu kwa watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi
vitakavyomsadia mjasiriamali kulingana na kazi anayofanya.
Shelukindo alimaliza kwa kuwapa
changamoto wajasiriamali kujitahidi zaidi sio tu kwa ajili ya kujishindia
ruzuku za programu ya“Safari Lager
Wezeshwa” lakini kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla. Aliwasihi
wajasiriamali na wafanyabiashara kwa ujumla kutega sikio kwa taarifa zaidi juu
ya usajili na kutembelea website ya www.wezeshwa.co.tz.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kusema, “Tunatoa
pongezikwa wajasiriamali kote Tanzania, Safari Lager inatambua na kuthamini
mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu. Tunatoa shukrani zetu za
dhati pia kwa wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba waendelee kuburudika na bia
hii inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio unaofanya tunawawezesha
wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia
kamili, inayodhihirisha mabingwa!.
No comments:
Post a Comment