Balozi wa kinywaji cha Hennessy Cyrile Gautier Auriol, akizungumza
na waandishi wa habari jana kuhusiana na mikakati yake ya kufanya
mazungumzo na wafanya biashara mbali mbali wa hapa nchini. Picha/ Mpiga Picha Wetu.
***************************
Na Mwandishi wetu
Balozi
wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier Auriol, yupo nchini kwa ajili
ya shughuli mbali mbali pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa jiji la
Dar es Salaam.
Auriol
aliwasili jijini juzi na kufanya mazungumza na wenyeji wake kabla ya
kuelezea nia ya safari yake ambayo lengo kubwa ni kutanua soko la
kinywaji hicho maarufu duniani kwa Watanzania nan chi za Afrika
Mashariki.
Alisema
kuwa pamoja na kukutana na wafanyabiashara, pia atakutana na watu wa
sekta tofauti, miongoni mwao ni wanamuziki na wanamitindo. Ziara ya balozi huyo itakuwa ya siku tano.
Alifafanua
kuwa ujio wake ni mara ya pili kwa ukanda wa Afrika Mashariki na ameona
kuna mafanikio makubwa kwa wafanyabiashara na hasa katika soko la
vinywaji vikali.
Alisema kuwa kinywaji cha Hennessy kwa sasa ndicho kinatamba katika ukanda huu na hivyo kuna haja kwa Watanzania kuanza
kupartavradha kwa ajili ya kujenga mwili na afya bora. Ikiwa na zaidi
ya historia ya miaka 250, Hennessy inatajwa kuwa kinywaji (Cognac) bora
zaidi duniani.
Pia Auriol
atakutana na wapenzi wa Hennessy katika matukio mbalimbali maalumu
ikiwemo chakula cha mchana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo baadhi
ya wanawake watakaochaguliwa watapata fursa ya kujifunza historia ya
kinywaji cha Hennessy lakini pia kuonja aina mbalimbali za kinywaji
hicho lengo likiwa kuwafundisha wanawake namna ya kufurahia kinywaji
hicho wakiwa majumbani mwao.
Balozi
Auriol pia atahudhuria chakula cha jioni na wafanyabiashara wa hapa
nchini katika mgahawa wa Akemi uliopo katika ghorofa la Diamond Jubilee.
Balozi Auriol atatoa elimu kuhusu Hennessy ikifuatiwa na uonjaji wa
kinywaji hicho pamoja na chakula kitakachoandaliwa na mpishi mkuu wa
hotel hiyo.
Ziara
ya balozi Auriol inaenda sambamba na juhudi nyingine za kutangaza
kinywaji hicho hapa nchini, mojawapo ikiwa ni kampeni ya mabango ya
‘Flaunt Your Taste’ yaliyosambaa jiji zima pamoja na ukamilishaji wa
chumba cha Hennessy kilicho katika Club 327, ambacho balozi Auriol
atakizindua.
Balozi
Auriol atakuwa na kikao maalumu pia na wapenzi wakubwa wa kinywaji
hicho, na pia atawazawadia mialiko maalumu ya kuingia kwenye klabu ya
wapenzi wa kinywaji hicho ya Afrika mashariki.
Pia
atatoa mafunzo maalumu kwa baadhi ya wahudumu kutoka katika bar kubwa
za jijini. Lengo kuu la mafunzo hayo yatakayofanyika katika hoteli ya
Southern Sun na George & Dragon ni kuwapa wahudumu ujuzi
utakaowawezesha kutoa huduma bora na ya kipekee kwa wateja wao wakati
wakiburudika na kinywaji cha Hennessy kwenye bar au hotel
wanazozipendelea.
No comments:
Post a Comment