HIVI NDIVYO VODACOM ILIVYO ZIPAMBANISHA TIMU ZA WABUNGE WA ZANZIBAR, MUUNGANO NA UGANDA SIKU YA MAPINDUZI
Ofisa
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Vodacom Hassan Saleh
akimkabidhi Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho
kombe lililotolewa na Vodacom kwa ajili ya mshindi wa mechi maalum kati
ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge wa Bunge la Tanzania
kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo huo ulichezwa
kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar na kufadhiliwa na Vodacom
Tanzania. Spika
wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akilikagua kombe
lililotolewa na Kampuni ya Vodacom kwa ajili ya mshindi wa mechi maalum
kati ya Timu ya Soka ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge wa
Bunge la Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo
huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar na kudhaminiwa na
Vodacom. Timu ya Bunge ilishinda bao moja kwa bila.
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Pandu Ameir Kificho
akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Soka ya Wabunge wa Bunge la Tanzania Amos
Makala amabe pia ni Naibu Waziri wa Habari,Vijana Utamduni na Michezo
kombe kufuatia kuichapa timu ya Baraza la Wawakilishi kwenye mechi
maalum ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katikati ni
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usamabazaji wa Vodacom Hassan Saleh waliodhamini
mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.
Kikosi cha Timu ya soka ya Wabunge wa Bunge la Tanzania kikiwa na kombe
muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa baada ya kuifunga timu ya Baraza
la Wawakilishi bao moja kwa bila kwenye mechi maalum ya kusherehekea
mika 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo huo ulidhaminiwa na kampuni ya
Vodacom.
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usamabazaji wa Vodacom Hassan Saleh akimpongeza
mchezaji wa timu ya Wabunge wa Bunge la Tanzania Adam Malima ambae pia
ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika mara baada ya kumalizka
kwa mechi yao dhidi ya Wajumbe wa Baraza La Wawakilishi kuadhimisha
miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.
Mechi hiyo ilidhaminiwa na Kampuni ya Vodacom.
Kikosi cha Timu ya Netiboli kinachoundwa na Wabunge wa Bunge la Uganda
kikiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kushuka uwanjani
kuvaana na kombaini ya Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Salum Mwalim
No comments:
Post a Comment