Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 2, 2014

cheka na pambano la urusi.


Awali ya yote napenda kuwapongeza na kuwatakia heri na fanaka ya mwaka mpya wa 2014.

pia ninamuomba mwenyezi mungu awape afya na nguvu mpya katika majukumu yanayow
akabili katika mwaka huu mpya.

Ndg waandishi organaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini tanzania TPBO-LTD,inawashukuru waandishi wote ambao wamehusika katika kuripoti taarifa za shughuri za tpbo katika mwaka uliopita,wapo ambao waliripoti kwa ufasaha na wapo ambao walilenga kutuingiza katika changamoto sizizo na uhakika kwa maslahi ya vyombo vyao kibiashara lakini yote hayo tpbo ilizichukulia kama ni promotion za kuikuza TPBO,ninawashukuru wote.


Sasa napenda kutowa ufafanuzi kuhusu kichwa cha habari hapo juu ili wale wanaoandika bila kutafuta ukweli wa mambo katika mwaka huu mpya wasirudie makosa yao ya kuandika habari za uzushi.


TPBO-LTD imekuwa ikishutumiwa na baadhi ya watu wasiojuwa hata taratibu za ngumu za kulipwa kuhusu safari ya bondia francis cheka kwenda kupigana nchini urusi hapo dec 21.


ukweli ni huu ambao mimi nauweka hadharani kwenu japo wengi wenu hamkuniomba nifanye hivyo.


Bondia francis cheka alituarifu mimi na rais wa PST ndg emanuel mlundwa kwamba anakabiliwa na matatizo makubwa sana ambayo yameathiri kwa kiasi kikubwa biashara zake za ujasiria mali na anadaiwa na Benki ya posta TPB ,Pia NMB, na kwamba nyumba yake nzuri ambayo ndiyo aliifanya dhamana katika mikopo hiyo ingeuzwa muda mfupi ujao ili kulipia deni hilo.


hivyo alitaka msaada wetu kama viongozi wake.


tulilichukuwa wazo na matatizo yake kwa uzito mkubwa sana ,hasa tukifikiria kwamba tutafanyeje ili kuokowa familia
yake.na matatzo ya kukosa makazi.

Kwa bahati nzuri haikuchukuwa muda mrefu wakala wa masumbwi raia wa kenya FRNKLYN IMBENZI alibahatika kupata pambano nchini russia lililomtaka bondia francis cheka akapambane huko pambano lisilo la ubingwa.

Kwa kweli hakukuwa na makubaliano kati ya francis cheka na wakala huyo IMBENZI kuhusu malipo,kwani imbenzi alimwambia cheka angelipwa usd 8000 tu.

Baada ya imbenzi kushindwana maelewano na cheka ilibidi ampatie namba yangu promota wa russia mr maxx ,


max alinipigia simu kuhusu azma yake ya kumpatia cheka pambano,na nikamwambia pesa ambazo anataka kumlipa cheka ni kidogo mno, promota aliongeza dola 2000 zaidi na kuwa dola 10000m za kimarekani.


Baada ya makubaliano hayo nilimuaru atume mkataba ,na alituma mkataba kweli kupitian e-mail yangu hii ninayoitumia.


kwa kuwa sikuwa na pesa za kulipia visa ya urussi kwa wakati ule,nilimpigia simu rais wa PST ndg emanuel mlundwa kumueleza kama anazo pesa za kumsaidia cheka apate visa na bima ya safari na amsaidie cheka.


mambo yote hayo wakati yanafanyika bondia mwenyewe francis cheka alitowa ushirikiano wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuongozana na rais wa PST mpaka ubalozi wa urusi kwa ajili ya kulipia visa na bima ya safari.


Kwa kuwa kiutaratibu mashirikisho mawili hayawezi kumuandikia kibali bondia kupigana nje ya nchi kwa pambano linalomhusu promota mmoja ,TPBO iliachia kazi ya kumpatia kibali cheka ifanywe na PST,Pia kwa ridhaa ya bondia mwenyewe cheka.


PST ilimpatia bondia cheka kibali na akaenda kupigana hali akijuwa wazi kwamba yeye ni bingwa na akijuwa matokeo mabaya hasa ya kupigwa KO yatagharimu ubingwa wake kupotea,


aliahidi angejitahidi kupigana kufa na kupona lakini bahati haikuwa upande wake kama siku zote amepoteza pambano na ubngwa,lakini ameweza kuyatatuwa matatizo makubwa yaliyomkabili na anaendelea kufanya kazi kama zamani kama mjasiria mali ,bondia mwenye kiwanda.


Naomba muelewe yote yaliyofanyika kuhusu bondia francis cheka tulikuwa tunayajadili kwa pamoja ,PST,TPBO,NA CHEKA MWENYEWE.


Ninashangazwa sana na kauli za watu wanaojifanya wana uchungu na bondia cheka kupoteza ubingwa wake ,nawauliza katika matatizo yaliyomkabili cheka ingekuwa wao ndiyo viongozi je wangeachia mali za bondia zipigwe mnada wa mabenki ili abaki na ubingwa hali wakijuwa wazi kwamba mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe? au walitaka bondia aadhirike na wamcheke?


TPBO-LTD inaamini kabisa kwamba katika ngumi za kulipwa kokote duniani bondia anajiwakilisha mwenyewe kama mfanyabiashara na haiwakilishi nchi kama watu wasioelewa wanavyotaka kuliingiza suala hili liwe la kisiasa wakati siyo pahala pake.


NGUMI ZA RIDHAA NDIZO HUWAKILISHA NCHI NA NDIYO MAANA ZINASAIDIWA NA SERILKALI KWA KIASI KIKUBWA SANA KOTE DUNIANI.


SIONI  KAMA KUNA  MTU AMBAYE ALIPASWA KULALAMIKA KWA CHEKA KUPOTEZA UBINGWA WAKE KAMA BABA YAKE MZAZI CHEKA, LAKINI ALITUSHUKURU SANA KWA KUMSAIDIA MTOTO WAKE KUPATA PESA ZA KULIPIA MIKOPO BENKI,NA AENDELEE NA BIASHARA ZAKE.


NA HATA CHEKA MWENYEWE ALISIKIKA KUPITIA REDIO CLOUDS AKITAMKA WAZIWAZI KWAMBA KAMA KUNA WATU WANADHANI MIKANDA YA UBINGWA INAPIKWA NA KUWA CHAKULA ,WAENDE AKAWAPATIE WAIFANYE CHAKULA,YEYE ANACHOHITAJI NI PESA KUTOKANA NA KAZI YAKE YA ULINGONI ,


TENA LA KUSHANGAZA ZAIDI NI KATIKA WANAOLALAMIKIA HILI WAMO MAPROMOTA MATAPELI WA KIMATAIFA AMBAO VYOMBO VYENU VIMEWARIPOTI KWA KUWADHULUMU MABONDIA WA KIGENI NA MPAKA KUKAMATWA NA POLISI.


KWA BAHATI MBAYA LEO HII BAADHI YA WAANDISHI WANAANDIKA HABARI ZAO ZA UPOTOSHAJI BILA HATA KUWAHIMIZA WALIPE MADENI YA MMAREKANI,NA WATANZANIA WANAOWADAI ,NAJIULIZA JE NI SABABU YA KITU KIDOGO?


NAWAKUMBUSHA NDG WAANDISHI KWAMBA UMAARUFU WA TPBO-LTD MMEUTENGENEZA NYINYI KUTOKANA NA KUSAIDIANA VYEMA KATIKA UPASHANAJI WA HABARI ,LAKINI ISIWE SABABU YA KILA LIFANYIKALO KWENYE NGUMI ZA KULIPWA NI TPBO-LTD


VIKO VYOMBO VINGINE VINAFANYA KAZI IFANYAZO TPBO-LTD.


TPBO-LTD INAAMINI KUWA;-


BONDIA FRNCIS CHEKA NA UMRI ZAIDI YA MIAKA 18


[1]BONDIA FRANCIS CHEKA ALISAINI MKATABA WA KUPIGANA RUSSIA BILA KULAZIMISHWA


[2] ALIKABIDHI PASSPORT KWA BALOZI WA URUSSI ILI AGONGEWE VISA BILA KULAZIMISHWA

 [3] BONDIA FRNCIS CHEKA ALICHUKUWA TAX TAREHE 17 DEC AKIELEKEA UWANJA WA NDEGE WA JULUS NYERERE HALI AKIWA NA AKILI TIMAMU NA HAKULAZIMIWHWA NA YEYOTE  [4]BONDIA FRANCIS CHEKA ALIINGIA NDANI YA NDEGE YA KLM BILA KULAZIMISHWA ,AKIJUWA WAZI ANAPITIA AMSTERDAM ,NA ATABADILISHA NDEGE PALE NA KUELEKEA URUSI KWA HIYARI YAKE MWENYEWE.

[5]BONDIA FRANCIS CHEKA ALIPANDA ULINGONI NCHINI RUSSIA KWA HIYARI YAKE MWENYEWE BILA KULOAZIMISHWA.NINAWAOMBA WOTE WANAOJARIBU KUUPOTOSHA UMMA KATIKA HILI WAWACHE KWANI UWONGO WAO HAUTAIBOMOWA TPBO-LTD.

BALI WANAIZIDISHIA UMAARUFU SANA.

WANAPOTEZA MUDA WAO BURE BILA MAFANIKIO


NA TPBO-LTD TUNAAMINI KABISA KWAMBA KUANDIKWA VIZURI AU KUSEMWA VIBAYA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI YOTE HAYO NI PROMOTIONS KWETU ,TUTAHESHIMU YOTE KATI YA HAYO DAIMA MILELE.

                          AHSANTENI SANA
                         IMELETWA KWENU NAMI;
                   YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA-USTAADH

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...