BAADHI ya wazee wa klabu ya Yanga wakizungumza na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Davis Mosha nyumbani kwake jana.
WAKATI zoezi la uchukuaji fomu za kuwania
uongozi katika klabu ya Yanga likianza leo, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa
klabu hiyo Davis Mosha amesema hana mpango ya kuwania nafasi yoyote katika
uchaguzi utakaofanyika Julai 15 mwaka huu.
Mosha alisema hayo
jana nyumbani wake Mikocheni jijini Dar es Salaam, akijibu maombi ya baraza la
wazee lililomuomba kugombea moja ya nafasi katika uchaguzi huo.
Alisema kwa sasa
hayuko tayari kugombea uongozi katika klabu lakini yupo tayari kusaidia kitu
chochote kinachohitajika kwa maendeleo ya klabu.
“NAshukuru wazee
wangu kwa kuja kuniaona na kunipa pole, pia nashukuru kwa kuona umuhimu wa mimi
kuwepo Yanga, lakini napenda niwaeleze kwamba sintoweza kuwania uongozi kwa
sasa, ila nipo tayari kuisaidia Yanga kwa lolote litakalokuwa ndani ya uwezo
wangu,”alisema.
“Mimi ni mpiganaji
kweli, naiopenda Yanga na napenda iwe na maendeleo…nitashirikiana na viongozi
watakaochaguliwa lakini mimi siwezi kuongoza Yanga kwa sasa nina mambo mengi ya
kufganya,”alisema
Mosha ambaye
alijitoa madarakani miezi michache kabla iongeza kuwa wanachama wa Yanga hawana
budi kuchagua viongozi ambao wapo tayari kuisaidia klabu hiyo na si kupata
chochote.
“Napenda
kuwahadharisha wanachama wenzangu nkwamba tusikurupuke, tutafute watu wenye
mapenzi ya kweli na si maslahi kwani Yanga ni kwa ajili ya kutumika si
kuvuna,”alisema.
Awali Katibu wa
baraza hilo Ibrahim Akilimali ‘Abramovich’ kwa niaba ya wazee wengine wa Yanga
ambao walikwenda nyumbani kwa Mosha kwa ajili ya kumpa pole kutokana na kufiwa
na Mkwewe, aliwasilisha ombi la kumtaka Mosha kurejea kundini.
Mzee Akilimali
alisema kuwa wameamua kumuomba Mosha arejee kuongoza Yanga kutokana na umahiri
mkubwa aliouonesha kipindi alichoongoza ambapo alikuwa mstari wa mbele kuisaidia
timu hiyo na hatimaye kwa kipindi kifupi iliweza kupata mafanikio.
“Mwanetu sisi wazee
wako tumekuja kukupa pole lakini pamoja na hilo tunakuomba urejee kuongoza kwani
bado tunakumbuka ushupavu wako katika kuongoza…kuna kombe la Kagame linakuja
ambalo wewe ulichangia kwa kiasi kikubwa kupatikana, sasa uje ulibakize tena
kombe hilo,”alisema Mzee Akilimali.
Aidha , Mzee
Akilimali aliongeza kuwa wanataka Yanga iingie kwenye mashindano na kushiriki
hivyo mchango wa Mosha katika hilo ni muhimu sana.
Uuchaguzi huo
utajaza nafasi za viongozi waliojiuzulu na ile ya mjumbe mmoja aliyefariki
dunia, ambapo viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa muda uliosalia
kama katiba inavyoelekeza na kwa mantiki hiyo viongozi hao watamaliza muda wao
wa miaka minne mwaka 2014.
Uchaguzi huo
unafuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti Lloyd Nchunga baada ya
kushinikizwa na baadhi ya wanachama wakiongozwa na baraza la wazee wa klabu hiyo
kutokana na kushindwa kuiletea mafanikio klabu hiyo chini ya uongozi
wake.
Pia nafasi ya
Makamu mwenyekiti iliyokuwa inashikiliwa na Davis Mosha ambaye alijitoa miezi
michache baada ya kuchaguliwa kutokana na kutoelewana na Nchunga, huku mjumbe
Theonest Rutashoborwa akitangulia mbele ya haki.
Uchaguzi huo pia
utajaza nafasi za Wajumbe walioachia ngazi ambao ni pamoja na Mzee Yusuf,
Charles Mgondo na Ally Mayay.
Kwa sasa Yanga imebaki na wajumbe wanne,
Mohammed Bhinda, Sarah Ramadhan, Tito Osoro na Salum Rupia ambao baada ya
uchaguzi wataungana na viongozi wapya na kuteua wajumbe wengine watatu kwa
mujibu wa katiba, hiyo inatokana na wajumbe hao wa kuteuliwa Seif Ahmed, Mbaraka
Igangula na Pascal Kihanga kujiuzulu.
Katika hatua
nyingine, wagombea wawili jana walijitokeza kuchukua fomu za kuwanmia nafasi ya
ujumbe katika, wanachama hao ni pamoja na Jumanne Mwamamwenye na Salehe
Hassan na Ayoub Nyenzi anayewania nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
No comments:
Post a Comment