Warembo waliokuwa wakiwania taji la Miss Kigamboni City 2012 wakicheza show ya ufunguzi jukwaani. |
Na Mwandishi Wetu
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar es Salaam, Edda
Silyvester, 21, usiku wa kuamkia juzi alifanikiwa kutangazwa kuwa
mshindi wa taji la kitongoji cha Kigamboni 'Redd's Miss Kigamboni 2012'
katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Navy Beach.
Kutokana na ushindi huo Edda alizawadiwa kitita cha Sh. 500,000
taslimu na mgeni rasmi katika shindano hilo, diwani wa Kata ya
Kigamboni, Dotto Msawa.
Nafasi ya pili katika shindano hilo lililopambwa na burudani safi
kutoka katika bendi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma
ilichukuliwa na Agnes Goodluck ambaye naye alipata zawadi ya Sh.
350,000.
Elizabeth Boniface alichaguliwa kuwa mshindi wa tatu na kupata
zawadi ya Sh. 300,000 huku nafasi ya nne ikienda kwa Esther Albert na
mshindi watano akiwa ni Khadija Kombo. Elizabeth na Khadija kila mmoja
alipata zawadi ya Sh. 200,000.
Jaji Mkuu wa shindano hilo, Benny Kisaka, alitangaza kuwa badala ya
warembo watatu atachukua warembo wote watano kwenda kushiriki katika
shindano la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.
Warembo wengine walioshiriki shindano hilo walikuwa ni Sophia
Martin, Rosemary Peter, Doreen Kweka na Linnah David waliambulia kitita
cha Sh. 150,000 kila mmoja.
Waratibu wa shindano hilo, kampuni ya K& L Media Solutions
wanawashukuru wadau wote waliosaidia kufanikisha shindano hilo
Kwa
kufanikisha onyesho hilo ambalo lilikuwa ni la mwisho kwenye kanda ya
Temeke.
No comments:
Post a Comment