Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la WWF, Jim Leape (wa pili kutoka kwa Makamu) na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam jana, Mei 31, 2012 kwa mazungumzo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirik la Kimataifa la WWF, Jim Leape (wa pili kushoto) na ujumbe wake, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Dar es Salaam jana Mei 31, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
amekutana na ujumbe wa Mfuko wa Dunia wa Kuhifadhi Maumbile (WWF) ambao
umeelezea nia yao ya kutaka kushirikiana na Serikali ya Tanzania
kuendeleza uvunaji endelevu wa raslimali asilia bila ya kuathiri mazingira.
Mkurugenzi
Mkuu wa WWF James Leape ambaye alifuatana na ujumbe wa watu watano
alimweleza Makamu wa Rais alipomtembelea ofisini kwake Ikulu jana, kuwa
mara nyingi miradi inayohusiana na raslimali asilia ikiwemo ya madini
inapotekelezwa husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira katika eneo
husika.
Alisema
tathmini ya athari kwa mazingira ni muhimu ili kuendeleza uchimbaji
endelevu wa madini hayo na kuiwezesha Tanzania kufanya vizuri katika
kilimo na hivyo kufanikisha malengo yake ya kufikia uchumi wa kijani.
Katika
mazungumzo hayo Makamu wa Rais alisema pamoja na
matatizo yaliyopo lakini wakati miradi inapoanzishwa suala la tathmini
ya mazingira huwa linapewa kipaumbele akitoa mifano ya miradi ya gesi
asilia ya Songo songo pamoja na ya chuma na makaa ya mawe iliyoko Ludewa
katika mkoa mpya wa Njombe.
Alisema
serikali inaamini kwamba miradi hiyo itaharakisha maendeleo kwa kuwa
itasaidia kufua umeme na hivyo kuwawezesha wananchi kupunguza matumizi
ya mkaa kwa kupikia na pia kupitia mgodi wa chuma kuna fursa ya kujenga
viwanda vya chuma kwa matumizi ya hapa nyumbani na kuuza nje ya nchi.
Aliuambia ujumbe huo kuwa suala la utunzaji wa mfumo wa ekolojia ni sera ya nchi na kusema
asilimia 40 ya eneo la nchi limehifadhiwa kwa ajili ya faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kuhusu
uchumi wa kijani, Dk. Bilal alisema serikali imejipanga vizuri kwa hilo
kwa kuwa tayari mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Ruvuma na Morogoro
inapewa uzito wa pekee kwenye suala la kilimo kwa lengo la kuiwezesha
nchi kufikia uchumi wa kijani.
No comments:
Post a Comment