Mkuu
wa Mkoa (RC) wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki ameitaka timu ya Taifa
ya Tanzania (Taifa Stars) kuiwakilisha vyema nchi katika mchezo wake
dhidi ya Msumbiji (The Mambas) utakaochezwa Jumapili (Juni 17 mwaka
huu).
Ametoa
mwito huo leo (Juni 14 mwaka huu) wakati akimkabidhi nahodha wa timu
hiyo Juma Kaseja, Bendera ya Taifa tayari kwa safari ya kwenda Msumbiji
itakayofanyika kesho (Juni 15 mwaka huu) asubuhi. Stars itaondoka kwa
ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi.
RC
amesema kiwango ambacho kilioneshwa na Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager kwenye mechi dhidi ya Ivory Coast na Gambia
kimerudisha imani ya Watanzania kwa timu hiyo, hivyo kuwataka wachezaji
kuendeleza moto huo.
Aliwataka
wachezaji wa timu hiyo pamoja na benchi la ufundi kupigana kiume
kuhakikisha wanashinda mechi hiyo, kwani ushindi mbali ya kuwaingiza
katika raundi inayofuata pia utaifanya Tanzania ipande kwenye orodha ya
viwango vya ubora duniani inayotolewa na Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA).
Mechi
hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar itafanyika kwenye
Uwanja wa Taifa ulioko Zampeto nje kidogo ya Jiji la Maputo kuanzia saa 9
kamili mchana kwa saa za huko.
Waamuzi
hao ni Hamada Nampiandraza atakayepuliza filimbi, Alberto
Razafitsatamy, Paulo Andriovoavonjy na Bruno Andriamiharisoa. Kamishna
wa mechi hiyo kutoka Botswana ni David Fani.
Taifa
Stars inaondoka na msafara wa watu 32 wakiwemo wachezaji, benchi la
ufundi na viongozi. Msafara huo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Shaibu
Nampunde.
|
No comments:
Post a Comment